JE SACCOS.pdf
Baada ya kufanya jitihada na mikutano mbalimbali hatimaye lile wazo la kuanzisha Saccos lililoletwa hapa JF hatimaye sasa imekuwa ni vitendo baada ya kufanikisha kupata usajili wa kudumu wa JE Saccos. Nipende kushukuru wanachama na kamati nzima kwa kuweza kufanikisha suala hili muhimu.
Pia shukrani zangu za dhati ziende pia kwa Ofisi ya Msajili wa Ushirika Tanzania na Afisa Ushirika Wilaya ya Kinondoni kwa jitihada za dhati za kupokea maombi yetu na kuyafanyia kazi.
Kamati ya Utendaji itaanza shughuli zake muda si mrefu baada mambo muhimu kuwa yamekamilika

Reply With Quote




Follow Us Here