Business & Economic ForumThis' a place where contributors with an interest in business or economics can "meet" and discuss issues of importance to the business and economics matters. Register to comment here!
Kama una CRDB Visa Card, na ulikuwa unafikiria kuitumia kwenye internet, basi usithubutu kutia sahihi kuiwezesha kutumika mtandaoni (ila kama tu unajua unachokifanya).
CRDB wametoa card mpya zenye nembo ya visa, ambayo wanatangaza kwamba unaweza kununulia vitu mtandaoni. Inaonekana kama ni bonge la wazo mpaka pale utakapogundua jinsi gani zisivyo salama hata kiduchu.
Mtu yeyote mwenye namba ya kadi yako, pamoja na vile vinamba vitatu vya "usalama" vilivyo nyuma, anaweza kuitumia hiyo kadi yako kwenye mtandao bila tatizo lolote. Kwa hiyo ukiitumia kwenye tovuti ambayo si salama, basi ni kama umegawa namba yako kwa watu wengine kujihudumia.
Pia ukiisahau kadi yako mezani, na mtu/rafiki yako/mtoto wako mtukutu/mpenzi wako/secretary wako akapata mda wa kunakili pembeni hizo namba zako, basi pia inakuwa imekula kwako.
Kama ulikuwa unafikiria ile pin yako, basi sahau maana haina kazi kwenye mtandao.
Address Verification
Unaweza ukawa unajiuliza mbona kuna watumiaji wengi tu wa credit cards duniani na wasiwe na wasiwasi hivyo?
Moja ya njia ambayo huwa inatumika kupunguza wizi wa kutumia kadi za wengine ni kufanya uhakiki wa anuani. Kiasi kwamba mtu akiweka oda ya kitu basi oda yake itakubaliwa na kadi kutumika ikiwa tu anuani ya ambapo vitu vya kwenye oda hiyo vitatumwa ni sawa na anuani ya mwenye kadi.
Kwa CRDB hii feature wameifinya, kiasi kwamba mtu yeyote duniani anaweza kutumia kadi yako na kununua na kutuma vitu vyake sehemu yoyote duniani anavyotaka.
Paypal
Kutumia site kama www.paypal.com inaweza kusaidia kuondoa uwezekano wa mtu kukuibia namba za kadi yako online.
Kujiunga kadi yako na paypal sio tatizo, tatizo ni jinsi ya paypal kuihakiki kwamba kweli ni ya kwako.
Paypal wanachofanya ni kukuchaji fedha kidogo (wastani wa 2,000TZS), halafa katika muamala huo wanaweka namba ya siri fulani. Sasa wewe inabidi uangalie statement yako kutoka benki, uione hiyo namba, halafu uwape paypal. Assumption hapo ni kwamba hakuna mtu mwingine anaweza kuona statement yako zaidi ya wewe.
Sasa ndani ya paypal unaweza ukakamilisha taratibu. Ukija CRDB ili kupata tu details za hiyo transaction, jasho litakutoka. Inaweza ukadhani ni kitu simple tu kupata details za transaction (hata mimi nilifikiria hivyo), lakini amini usiamini utashangazwa ... Nimefanya si chini ya trip 10 kwenda CRDB kwa ishu hiii, usihesabu simu, na nimetoka kupiga nyingine sasa hivi ... lol ...
Ningetakiwa niwe nimeshakata tamaa ila tu nataka tu nifuatilie mpaka mwisho waniambie inawezekana au haiwezekani.
Ila kama huu ndio utaratibu, sioni ni jinsi gani wataweza kuwahudumia wateja hata 100 tu wanaotaka kujiunga na paypal. Achilia mbali kwamba hawa watu 100 inabidi wapige kwata CRDB more that 10 times, halafu wawe wanapiga simu mara kwa mara kuwakumbushia CRDB case zao. Na mara nyingi watu unaoongea nao CRDB hata hawaelewi unazungumzia nini.
Makubaliano yako na CRDB ni soo
Ili kuiruhusu kadi yako kutumika online, itabidi utie saini makubaliano yako na CRDB, ambayo yanavipengele ambavyo vinaiondolea CRDB jukumu lolote la kukuhakikishia usalama wako unpotumia kadi yako kwenye mtandao. Kwa hiyo ukiwa online na kadi yako, jua you are on your own.
Kwa watumiaji wengine duniani kuna taratibu za jinsi ya mtu kupinga kuchajiwa transaction ambazo hujazifanya wewe. Na kuna taratibu za jinsi gani utarudishiwa pesa zako.
Mpkataba wa CRDB hauoneshi kama kuna kitu kama hicho. Kwa hiyo mtu akipata details za kadi yako, siku zote itakuwa inakula upande wako.
Kwa hiyo baada ya kuutia saini tu nimehakikisha kadi yangu haiondoki machoni pangu, na pia nahakikisha akaunti hiyo ya CRDB haina vijisenti vingi ... mpaka ntakapomaliza hii exercise.
Hitimisho
Sasa hivi unaweza kutumia kadi yako ya CRDB kwenye mtandao, lakini you do it at your own risk, tena risk kubwa tu.
Kinachonitisha ni kwamba kama kadi yako imewezeshwa kutumika kwenye internet, mtu hana haja ya kukuibia kadi nzima kwa sababu utashtuka, utaripoti, na kadi itafungwa. Anachotakiwa kufanya ni kupata namba za kadi zilizopo mbele, na vile vijinamba vitatu vilivyopo nyuma ya kadi, na inakula upande wako kimya kimya.
Kama umeiwezesha kadi yako kutumika kwenye mtandao, na kama vijinsenti vyako kwenye akaunti yako sio vidogo, na kama huwezi kuitunza details za kadi kiasi hicho, ni vyema ungewaambia waizibe isitumike kwenye mtandao ... or u may have to learn the hard way.
__________________
There are only 10 types of people in the world. Those that understand binary, and those that don't.
Re: CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao
Kuna siku nilikuwa German, nikatumia CRDB viza card kulipa, wakaniambia mtandao haujajibu. Nikaacha, nikiwa naendelea na manunuzi yangu ktk duka hilo hilo, nikaitwa na yule mhudumu, huku akinionesha risiti ya malipo yangu ambayo mtandao wa CRDB ulikataa mara ya kwanza. Fikiria kama ningeondoka ktk duka lile ingekuwaje? Tusikatae ushauri, ni vizuri tukachukua tahadhali kabla ya hatari.
Re: CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao
Ahsante sana Manitoba. Umeanzisha thread nzuri ambayo naamini itatusaidia wengi. Mimi mwenyewe nimeshachukua hiyo card ila nilikuwa nasitasita kuitumia online kwa sababu zinazokaribiana na hizo, ukifika pale customer care CRDB M.City utacheka sana!! Kuna yule dada anayetoa kadi za visa, Mungu wangu, yaani hajui hata maana ya 'online transaction'' yeye anachojua ni ''kadi za internet'' basi!!!! Mi nilimuuliza maswali mawili matatu kuhusu matumizi ya kadi hizi nikagundua kuwa ndo kwanza nampa misamiati ambayo hajawahi kusikia, basi nikaamua kumwacha na kuchukua kadi, mengine nilijua mbele kwa mbele. All in all CRDB hawajajipanga na hizi card. Kama wafanyakazi wenyewe hawajui linaloendelea, itakuwaje ukienda na tatizo la fraud???????
Kwa hili CRDB wamepiga hatua, ila nafikiri cost ya hii kitu itakuwa ni kubwa zaidi ya Benefit. Cha kufanya kwa wale wenye kutaka huduma hii ni bora kuwa na account mbili yaani Moja ni kwa ajili ya transaction za online, unahamisha pesa na kufanya transactions on spot, hapo hapo. Nyingine ni kuhifadhia pesa kama una wasiwasi
Huu nafikiri ni ushauri mzuri. Kuwa na Account mbili. Moja kwa ajili ya kuhifadhia VGcent vyako na ya pili maalumu kwa ajili ya Online Transactions ambapo unaweka hela pale tu unapotaka kufanya manunuzi on line. yes, nadhani hii ni njia bora wakati tukiendelea kusubiri uboreshaji wa huduma hii muhimu sana...!
Mkuu, inaonyesha wewe umesome tu kwenye shule kuhusu credit cards. Mimi siyo mtalaamu wa uchumi wala mtu wa banki, ila nimetumia CC kadhaa. Labda siwezi kueleza zaidi kwa sababu hiyo. Ila kuhusu wizi kwa credits cards na compensation unaweza check hapa upate info zaidi ya ile niliyokupatia. <http://en.wikipedia.org/wiki/Credit_card_fraud>
Huyu jamaa pamoja na huyu <http://www.securityfocus.com/news/11493> wanakuambia kuwa ni hela nyingi sana zinaibiwa Duniani kwa CC kila mwaka. Hao wote si CRDB. SOma kwa makini sana.
Inawezekana sijaenda hata shule kaka ... lol ... I am fine with that ... Ila turudi kwenye mada ...
Sawa fedha nyingi zinaibwa kwa CC. Kitu kimoja ambacho hujajiuliza ni kwamba hizo pesa zinazoibwa mwisho wa siku ni hasara ya nani? Wewe moja kwa moja uaka-assume mwenye kadi ndio anakula hasara.
Labda nikusaidie kufikiri kidogo. Kama yote hiyo ingekuwa na hasara ya wenye kadi, basi concept ya "Charge Back" isingekuwa ina-exists, au ingebaki ni pambo tu. The fact kwamba concept ya "Charge Back" iko mpaka kwenye sheria za wenzetu, ingekufanya labda ufikiri kwamba wapo watu wanaorudishiwa pesa zao pindi kunapotekea fraud. Hiyo ingepelekea ufikirie kwamba kama wapo wanaorudishiwa pesa hizi, basi pengine hasara hiyo yote si ya mwenye kadi tu, bali ni ya yule anayemrudishia mwenye kadi. Na pengine ungejiuliza swali zuri sana: hizo pesa anazorudishiwa mwenye kadi baada ya fraud, zinatoka kwa nani? Hiyo ingekupelekea kutafuta ukweli wa ni nani hasa anayekula hiyo asara baada ya pesa kuibwa na mwenye kadi kurudishiwa.
Hivi hiyo linki uliyotusaidia ( Credit card fraud - Wikipedia, the free encyclopedia ) umeisoma? Mbona inajieleza vizuri tu? Labda line hii hapa ulii-skip "Merchants in high-risk industries anticipate a certain amount of credit card fraud, and set prices accordingly. These higher costs are then passed onto the customer". Does that make u rethink your beliefs about who caries the burden of the stolen money? I hope u see that its not really the card holder. (at least not directly).
Au hii line uliiona kwenye hiyo tovuti uliyotupatia: "In the case of fraud, the merchant and not the credit card company pays the full cost of the fraud plus a chargeback fee or the merchant's chargeback insurance covers it. In addition credit card companies have to pay for preventing fraud while maintaining a good customer experience."
Kama bado inakupashida kuona: wenye kadi wengi huwa wanarudishiwa pesa zao. Kama wewe kwa experience yako ulishawahi kuibiwa na mtu aliyetumia CC yako na ukakaa kimya, basi pole. Lakini wenzako wengi huwa wana-comlain na kurudishiwa.
Hatubishani ila tunaongelea kwa uzoefu wa kutumia na si kusoma shule na pia kupeana ujumbe kwa kutumia experience. Siwateti CRDB kwa namna yoyote ile na CRDB hawawezi kufanana na Inter-national companies za America au Europe za CC. Pia pamoja na kuwa kuna hiyo disclamer kwa CRDB nimewahi fanya makosa ya k-transaction kwa tune ya equivalent ya 500,000TSHS. Nili-report international Banking section pale CRDB TZ wakarekebisha in three days.
Exactly my brother. Point mojawapo niliyokuwa nataka kuweka ni kwamba hawafanani. Na moja ya tofauti ni kwamba safety yako kwa kadi ya CRDB ni ndogo kuliko ya hao. Kama unadhani hapo nimekosea, basi niambie nimekosea. Wapo waliojibu hii mada waking'ang'ania kwamba wanafana na kwamba term CRDB Visa Card hazina tofauti na nyingine zote "duniani", wakati mtu clearly unaweza kuona kwamba kuna tofauti.
Kama wewe ni mzoefu wa kutumia CC, basi ni vizuri. Na kama ulikuwa hujui kwamba issuer wako huko anachukua steps kukulinda, sio kosa lako. Lakini pengine ungejua hivyo ungeona tofauti na CRDB.
Bottom line, tumia hiyo card huku ukijua kwamba uking'atwa hakuna msaada kutoka CRDB. Na sisemi kwamba CRDB lazima ifanane na hao wengine, la hasha. Ninachosema ni kwamba wewe mtumiaji ujua kuna tofauti, pengine kubwa tu.
Ila ninasema kwamba wako sawa sawa kulingana u-TZ kule. Wata-improve tu service zao with time. Sio muda wa kuanza kwaponda kuwa wao nyuma na hawajali rights za wateja wao. Kuna banks kadhaa za SEA zina masharti magumu sana na nilishangaa sana jinsi wateja wanavyo-chargiwa services a hizo benks ukifananisha na Europe au TZ na jinsi wanavyolalamika sana. Lakini bankers wana sababu.
I hope humaanishi kwamba kama mtu akiona matatizo basi akae kimya tu na kuamini kwamba wata"improve tu service zao with time". Maana fikira kama hizo ndio chanzo kimojawapo cha umasikini wetu.
Halafu naomba kama ungekuwa na mda urudie maandiko yangu yote halafu unionyeshe wapi nimewaponda CRDB. CRDB ni benk kubwa yenye heshima TZ, sasa mimi nani nisiye na hata kibanda kuwaponda? Lakini kwa upande mwingine, sioni kwa nini unadhani natakiwa nikae kimya nikiona kuna tatizo. Kwani ni uongo kwamba hawajali maslahi za wateja wao kwa upande huu wa hizi kadi?
Nimeshatoa mifano kadhaa ya jinsi wengine wanavyofanya kuhakikisha kwamba mwenye kadi inalindwa. Na hizi steps ni standard, zinajulikana, na Visa Internation supports them. Sasa kwa CRDB kuchagua kutochukua hata moja ya hizi steps kunanifanya niamini kwamba hawajajali maslahi ya wateja wao katika hili. Na nimesaini kale kamkataba nikijua hilo. Na nikiibiwa kuna uwezekano mkubwa sitaangaika kuwa-contact CRDB kwa nia ya kurudishiwa pesa zangu. Ila point niliyotaka kuweka, ambayo kaka naona unairuka na kudhani nataka kuwaponda CRDB, ni kwamba wewe mteja unayetumia kadi ya CRDB ujue ukweli ulivyo.
Na naomba nisisitize: sijasema CRDB lazima achukue hizi steps, la hasha! Wao ni wafanyabiashara, na hiyo ni biashara yao. Na nilikuwa nalijua hilo wakati natiasaini kale kamkataba. Ninachosema ni kwamba CRDB hawajachukua hizi hatua.
Kama ninasema uongo niambie, lakini usinihukumu kwa ambacho sijasema.
Tujitahidi kupenda home na vitu vya home. Vilivyo majuu havikushuka. Vilianza hivi hivi.
Nafurahi kusikia kwamba wewe ni mmoja wa wanaopenda vya nyumbani. Labda nikufundishe kitu kimoja. Huko kwa wenzetu havikushuka, lakini unajua vilikujaje? Vilikuja kwa sababu consumers walikuwa wanapigia kelele huduma ambazo hawaridhiki nazo.
Kweli havikushuka, lakini havikuja kutokana na watu kukaa kimya hoping kwamba vitu vita-improve vyenyewe. Unadhani huko kwa wenzetu hao card issuer walipenda interests za mwenye kadi zilindwe kisheria? No they didnt. Na kama nchi zao zingekuwa zimejaa watu wanaosema "tusubiri tu with time vitu vita improve", then usingekuta sheria kama hizo zimepitishwa.
Penda vya nyumbani, na usisahau kudai ubora. Utakuwa unajisaidia wewe na nchi yako. Na hata huyo bepari wako in the long run.
Take home message: Shule ina umuhimu wake. Ila uzoefu wa siku nyingi una umuhimu zaidi. Rubani aliyekuwa trained kuendesha Boeings za abiria mwaka jana, hawezi kuanza na 747-400 immediately. Lazima aanzie chini kwenye 737-200 kwanza!
Du! mzee naona umenikaba kweli kwenye hilo la shule. Sijui nini kumekufanya ufikirie kwamba hata nimeenda shule kihivyo basi. Elimu ya muhimu niliyonayo ni kusoma na kuandika kiswahili, na ka-kingereza ka kishkaji. Tofauti yetu labda ni kwamba napenda kufuatilia zaidi na kuujua ukweli kuliko kutegemea tu experience yangu.
Na tofauti nyingine ni kwamba nikikupa reference (website, kitabu etc) mimi ninakuwa nimeisoma na kujaribu kadiri ninavyoweza kuielewa ... hapa am just teasing u man ... don't get all red on me
Tukirudi kwenye mada ... hata mimi ntaitumia kadi ya CRDB. Nimeona niseme hivi kwasababu muheshimiwa na wachache wengine wanadhani ninasema "CRDB should close this service" au "CRDB has done a really bad job". Ila Ninajua risk zake fika, na ninajua jinsi ya kuzipunguza. Na ningependa mtu mwingine yeyote azijue kwanza. Na kwasababu CRDB inazitangaza tu bila kusema chochote kuhusu risks zake, wasiwasi wangu ni kuna watu wataingia bila kuzijua risks na kuanza kulalama baadaye.
Kama wewe unawaambia watu hakuna tatizo kwa sababu ya experience yako, nadhani basi only time will tell ... napenda kuwa proven wrong, kwa sababu ndio jinsi rahisi yakunikumbusha ujinga wangu ...
__________________
There are only 10 types of people in the world. Those that understand binary, and those that don't.
Kuna siku nilikuwa German, nikatumia CRDB viza card kulipa, wakaniambia mtandao haujajibu. Nikaacha, nikiwa naendelea na manunuzi yangu ktk duka hilo hilo, nikaitwa na yule mhudumu, huku akinionesha risiti ya malipo yangu ambayo mtandao wa CRDB ulikataa mara ya kwanza. Fikiria kama ningeondoka ktk duka lile ingekuwaje? Tusikatae ushauri, ni vizuri tukachukua tahadhali kabla ya hatari.
Kwa kesi kama hii, na kam ungeondoka bila hata kuchukua kitu, kale kamkataba ka CRDB kanasema "utajiju".
Lakini kwa wenzetu, zipo taratibu rahisi za kufuta ili urudishiwe pesa zako.
__________________
There are only 10 types of people in the world. Those that understand binary, and those that don't.
Ahsante sana Manitoba. Umeanzisha thread nzuri ambayo naamini itatusaidia wengi. Mimi mwenyewe nimeshachukua hiyo card ila nilikuwa nasitasita kuitumia online kwa sababu zinazokaribiana na hizo, ukifika pale customer care CRDB M.City utacheka sana!! Kuna yule dada anayetoa kadi za visa, Mungu wangu, yaani hajui hata maana ya 'online transaction'' yeye anachojua ni ''kadi za internet'' basi!!!! Mi nilimuuliza maswali mawili matatu kuhusu matumizi ya kadi hizi nikagundua kuwa ndo kwanza nampa misamiati ambayo hajawahi kusikia, basi nikaamua kumwacha na kuchukua kadi, mengine nilijua mbele kwa mbele. All in all CRDB hawajajipanga na hizi card. Kama wafanyakazi wenyewe hawajui linaloendelea, itakuwaje ukienda na tatizo la fraud???????
lol
Mimi siwezi kuwalaumu wale wahudumu kwa kweli. Wao wamepewa kazi ya kufanya, na pengine wanaifanya kadiri ya uwezo wao (ingawa uwezo wao unaweza ukawa limited kidogo).
Mimi tawi langu ni pale Azikiwe kabisa, nadhani ndio makao makuu na ninajitahidi kupiga kwata pale tu.
Kuna dada pale ndio ana-deal na hizi card, kwa kweli anajitahidi. Huwa nnapataga hasira sana, lakini baadaye nikifikiria naona kweli si kosa lake.
Mfano mimi mpaka kuwa na hii kadi ikifanya kazi jasho lilinitoka.
Siku ya kwenda kuchukua nikauliza mara mbili-mbili, "kwa hiyo ipo tayari kuitumia kwenye internet?", kwa sababu ndio sababu pekee kwa nini nilitaka kadi ya CRDB. Nikajibiwa "ndio". Kwenda kujaribu ikagoma, ikisema issuer amegome contact your issuing bank. Nikawanendea, ndio wakaniambia sasa kwamba inabidi ujaze kamkataba ... lol
Haya nikajaza mkataba, nikauliza baada ya mda gani itakuwa tayari, wakaniambia siku mbili. Baada ya siku tatu nikajaribu, ikagoma tena. Nikarudi tena. Yule dada akawauliza watu wa "Card Center" nadhani ambao ndio ma experts sasa. Sasa sijui hiyo fomu yangu ikawa imepotea au ilikuwaje. Nikaambiwa nijaze nyingine. It was clear lakini kwamba halikuwa kosa la yule dada.
Haya nikajaza fomu nyingine ya kale kamkataba. Nikauliza tena "siku ngapi?", "mbili". Baada ya siku nne nikajaribu ikagoma tena. Nikarudi tena CRDB, yule dada akaongea tena na Card Center ... nikaambiwa baada ya siku 2 itakuwa tayari ...
Baada ya siku 3, guess what? ikagoma.
Baada ya kurudi tena mara 2, ndio nikaambiwa sasa kwamba kadi yangu namba zake ziko kwenye range ya kadi zenye matatizo, kwa hiyo inabidi niombe nyingine ...
Kweli baada ya kuomba kadi nyingine, ikakubali ... miezi 4 baada ya kuanza process ya kuomba kadi.
Na trip zote nilikuwa narudi pale ilikuwa inabidi nijaribu kuwaelewesha kwa nini ninafikiri tatizo ni lakwao na sio langu. Saa nyingine nilikuwa nakereka mpaka nilikuwa nawapa offer waitumie wao kadi hiyo kwenye mtandao waangalie kama inafanya kazi, maana mi nawaambia haifanyi kazi wao wananing'ang'anizia inafanya.
Sasa hivi napata shida kupata details ya transaction moja tu ya sh 2,579TZS iliyofanyika october mwaka jana. Na nashindwa kupata. Je, ingekuwa case ya kuibiwa hizo fedha ingekuwaje?
__________________
There are only 10 types of people in the world. Those that understand binary, and those that don't.
Re: CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao
am not sure which card these guys are talking about,But if it's the one with 4 digit passcode then that is a BIG NO NO!!do not use it online,especially in "not so obvious websites"
online banking and security is a HUGE issue,kuna part ya vendor wa kadi yako na part yako.
part ya vendor insures that they have strongest encryption mechanisms possible on their passcodes..,puting a 6 digit code is a way 2 go. not four.it takes less than 7 mins to break any 4 coded password and use it.vendors pia has to make sure their site has what it takes for a safe online precense ya wateja wake
a quick look at their website reveals that they are not that serious with security
that RC4 128bit encryption they are using is Ok but not top of the line.security is a very serious matter and it needs highest level of dedication and seriousness.
BUT that aint all,the biggest problem is actually on consumer side.
buying stuffs online especially through websites is a huge toll for average tanzanian consumers,most people are using pirated anti viruses and antispywares which are loaded with enough malaware(s) than they can think of.good thing that Tanzanian shopping online do not excite that many phishers.but with economic improvements that could be another case.
all in all this is a fantastic move by CRDB that needs cleaning up,shining a lil bit and clear some dusts.
taking care of encryption issues,moving that 4 coded password a step higher or give users a more viable solutions like hardware encrypted password alternative etc.
__________________
"I may not agree with you. However, I will defend your right to express your opinion"
Re: CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao
CRDB ni benki kubwa na ina uwezo wa kurekebisha mambo mengi haraka kwa kutumia wataalamu wa hali ya juu, uwezo wa kulipa wanao (angalia faida zao kwa mwaka) Lakini kwa uzoefu wa mahusiano na CRDB, kwenye hizo card na katika huduma nyingine hata kuwaangalia tu wanavyoendesha mambo yao ninaona mapungufu katika "creativity na entrepreneurship". Wana tatizo la kuwa wakubwa kiasi kwamba ni kazi kubwa kwao "kuona tatizo na kulirekebisha".
Nimekwisha hangaika sana na hiyo kadi yao nikiwa safarini na niliifutilia mbali kwa sababu nilipowaambia hata hawakujali, ili nisiendelee kugombana nao nikarudi kwenye huduma ya kawaida. Nilikwenda huko kwenye kadi kwa vile nilijua ni huduma nzuri na inahitajika.
Ninakumbuka kuna wakati ilikuwa ukiweka fedha kwenye account ya mtu mwingine walikuwa wanakuchaji, wakati wenzao walikuwa wamekwisha acha -wao walikuwa bado wanaendelea, mimi niliendelea kuwauliza na hawakuwa na majibu ya kufanya chochote. Miaka mitatu baadaye ndio wanabadili (baada ya baadhi yetu kuamua kutumia banki nyingine kutuma vipesa kidogo kwa wazee wetu.
Tatizo la CRDB
- Hawana mfumo wa "continous improvement system"
- Mafanikio yemewalevya hawasikilizi la mtu.
- NAdhani kuna mapungufu katika utafutaji wa wataalamu au mifumo mizuri ya kufanyia kazi.
NA WAO WANUWEZO WA KULIPIA GHARAMA ZA HUDUMA NZURI KULIKO WENGINE.
Wamekuwa wakubwa bila ya kuwa na mfumo wa uongozi, utawala, usimamizi unaoendana na shughuli zao, ndio maana wanaweka hao akina dada kuhudumia madesk ya hizo kadi wakati wenyewe uelewa wao ni kidunchu kuhusu hizo kadi -Sasa customer service gani hiyo??????????????
- Angalia hata ATM zao, ukienda ATM mara 10, mara nne hutapata huduma, ni mwaka wa ngapi toka wameweka hizo ATM, bado hawajajifunza tu???? Je wanahamu ya kujifunza?????
- Ni vyema CRDB ikawa tayari kujifunza na kusikiliza, nakumbuka mwandishi mmoja wa "daily noise" aliandika siku moja "CRDB Bank, the bank that listens...but does not do anything"
-
- Kufanikiwa kwao si lazima ni kwa vile ni wazuri katika "business management" la ni kwa vile tu wapo mahali sahihi wakati mwafaka na connections nzuri.
- Hivi tumekwisha jiuliza kwa nini vibenki vidogo kutoka kenya vimefungua matawi hapa na crdb wapo bongo tu???????????????? mimi sijui lakini inakupa kawasiwasi ka kukosa "drive"
Mimi siwezi kuwalaumu wale wahudumu kwa kweli. Wao wamepewa kazi ya kufanya, na pengine wanaifanya kadiri ya uwezo wao (ingawa uwezo wao unaweza ukawa limited kidogo).
Mimi tawi langu ni pale Azikiwe kabisa, nadhani ndio makao makuu na ninajitahidi kupiga kwata pale tu.
Kuna dada pale ndio ana-deal na hizi card, kwa kweli anajitahidi. Huwa nnapataga hasira sana, lakini baadaye nikifikiria naona kweli si kosa lake.
Mfano mimi mpaka kuwa na hii kadi ikifanya kazi jasho lilinitoka.
Siku ya kwenda kuchukua nikauliza mara mbili-mbili, "kwa hiyo ipo tayari kuitumia kwenye internet?", kwa sababu ndio sababu pekee kwa nini nilitaka kadi ya CRDB. Nikajibiwa "ndio". Kwenda kujaribu ikagoma, ikisema issuer amegome contact your issuing bank. Nikawanendea, ndio wakaniambia sasa kwamba inabidi ujaze kamkataba ... lol
Haya nikajaza mkataba, nikauliza baada ya mda gani itakuwa tayari, wakaniambia siku mbili. Baada ya siku tatu nikajaribu, ikagoma tena. Nikarudi tena. Yule dada akawauliza watu wa "Card Center" nadhani ambao ndio ma experts sasa. Sasa sijui hiyo fomu yangu ikawa imepotea au ilikuwaje. Nikaambiwa nijaze nyingine. It was clear lakini kwamba halikuwa kosa la yule dada.
Haya nikajaza fomu nyingine ya kale kamkataba. Nikauliza tena "siku ngapi?", "mbili". Baada ya siku nne nikajaribu ikagoma tena. Nikarudi tena CRDB, yule dada akaongea tena na Card Center ... nikaambiwa baada ya siku 2 itakuwa tayari ...
Baada ya siku 3, guess what? ikagoma.
Baada ya kurudi tena mara 2, ndio nikaambiwa sasa kwamba kadi yangu namba zake ziko kwenye range ya kadi zenye matatizo, kwa hiyo inabidi niombe nyingine ...
Kweli baada ya kuomba kadi nyingine, ikakubali ... miezi 4 baada ya kuanza process ya kuomba kadi.
Na trip zote nilikuwa narudi pale ilikuwa inabidi nijaribu kuwaelewesha kwa nini ninafikiri tatizo ni lakwao na sio langu. Saa nyingine nilikuwa nakereka mpaka nilikuwa nawapa offer waitumie wao kadi hiyo kwenye mtandao waangalie kama inafanya kazi, maana mi nawaambia haifanyi kazi wao wananing'ang'anizia inafanya.
Sasa hivi napata shida kupata details ya transaction moja tu ya sh 2,579TZS iliyofanyika october mwaka jana. Na nashindwa kupata. Je, ingekuwa case ya kuibiwa hizo fedha ingekuwaje?
Aisii hongera sana muheshimiwa, inaonekana umepigana vita kubwa tofauti yako na mimi ni kuwa wewe umeishinda, mimi imenishinda kabisa!! kila nikijaribu kununua kitu online inaniambia kuwa hakuna communication na bank, nifanyeje ndugu ili nami nifanikiwe? nina midude kibao ya kununua lakini ndo hivo tena kadi inagoma. plz help me out!!
Kutumia card ya CRDB kwenye mtandao ni wazo zuri. Na CRDB inabidi wapongezwe kwa hatu hiyo.
Ninachosema hapa ni kwamba CRDB wamejitoa kwenye tatizo lolote litakalotokea kwa matumizi ya kadi yako. Kitu ambacho ni tofauti na kwa wenzetu kwa jinsi ninavyofahamu mimi.
Hiyo inafanya matumizi ya hii card yawe na risk zaidi. Yaani hata kama kosa ni lakwao bado hakuna wa kukusaidia.
Kwa mfano ukinunua kitu online halafu kwa bahati mbaya anayekuuzia akatoa fedha zaidi ya zile alizotakiwa kutoa. Halafu kwa bahati mbaya akawa anasuasua kukurudishia fedha zako. Hapo utakuwa huna jinsi ila kukubali umeliwa kimachomacho. Lakini kwa wenzetu kuna taratibu za kupinga transaction ambayo si sawa au si halali, na mwenye kadi waweza kurudishiwa pesa ambazo hukutakiwa kukatwa. Kwa CRDB inaonekana hakuna kitu kama hicho.
Sisemi kwamba CRDB wanatakiwa waweke utaratibu kama huo. Ila nasema wewe mtumiaji ujue hali ilivyo, usije ukang'atwa siku ndio ukaanza kutoa macho na kuwa mkali na CRDB.
Manitoba,
Nadhani usitegemee hata siku moja mfanyabiashara yeyote atakuwa tayari kubeba mzigo wa hasara ambao anajua unaweza kumwangukia. Ninavyofahamu mimi nikuwa transaction zinazofanywa kwenye credit card zinabeba amount kiasi kwa ajili ya ku-cover insurance kwa upande wa benki au taasisi inayohusika. Iko haja ya kufanya research na kuona kama CRDB ina insurance kwenye credit card zake,
Nafikiri kwa vile ndiyo mfumo umeanza kutumiwa na moja ya benki zetu basi CRDB waongeze kasi ya kuuboresha kwa ni mfumo mzuri na wakistaarabu sana. Inakadiriwa katika kipndi cha mwaka 2004 biashara iliyofanyika kupitia kwenye internet huko Marekani ilifikia dola bilioni 70. Ni wazi kuwa huu mfumo unachukua nafasi kubwa katika kufanya biashara.
CRDB wachukue haya kama changamoto.
__________________
'Tough times never last but tough people do' Dr. Robert Schuller