CRDB Visa Card: Utata wa matumizi yake mtandaoni - Page 2 - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Business & Economic Forum


Business & Economic Forum This' a place where contributors with an interest in business or economics can "meet" and discuss issues of importance to the business and economics matters. Register to comment here!


Reply
 
LinkBack Thread Tools Rate Thread Display Modes
Old 19th January 2009, 11:05 AM  
CRDB Visa Card: Utata wa matumizi yake mtandaoni
Manitoba Manitoba is offline 19th January 2009, 11:05 AM

Kama una CRDB Visa Card, na ulikuwa unafikiria kuitumia kwenye internet, basi usithubutu kutia sahihi kuiwezesha kutumika mtandaoni (ila kama tu unajua unachokifanya).

CRDB wametoa card mpya zenye nembo ya visa, ambayo wanatangaza kwamba unaweza kununulia vitu mtandaoni. Inaonekana kama ni bonge la wazo mpaka pale utakapogundua jinsi gani zisivyo salama hata kiduchu.

Mtu yeyote mwenye namba ya kadi yako, pamoja na vile vinamba vitatu vya "usalama" vilivyo nyuma, anaweza kuitumia hiyo kadi yako kwenye mtandao bila tatizo lolote. Kwa hiyo ukiitumia kwenye tovuti ambayo si salama, basi ni kama umegawa namba yako kwa watu wengine kujihudumia.

Pia ukiisahau kadi yako mezani, na mtu/rafiki yako/mtoto wako mtukutu/mpenzi wako/secretary wako akapata mda wa kunakili pembeni hizo namba zako, basi pia inakuwa imekula kwako.

Kama ulikuwa unafikiria ile pin yako, basi sahau maana haina kazi kwenye mtandao.

Address Verification
Unaweza ukawa unajiuliza mbona kuna watumiaji wengi tu wa credit cards duniani na wasiwe na wasiwasi hivyo?

Moja ya njia ambayo huwa inatumika kupunguza wizi wa kutumia kadi za wengine ni kufanya uhakiki wa anuani. Kiasi kwamba mtu akiweka oda ya kitu basi oda yake itakubaliwa na kadi kutumika ikiwa tu anuani ya ambapo vitu vya kwenye oda hiyo vitatumwa ni sawa na anuani ya mwenye kadi.

Kwa CRDB hii feature wameifinya, kiasi kwamba mtu yeyote duniani anaweza kutumia kadi yako na kununua na kutuma vitu vyake sehemu yoyote duniani anavyotaka.

Paypal
Kutumia site kama www.paypal.com inaweza kusaidia kuondoa uwezekano wa mtu kukuibia namba za kadi yako online.

Kujiunga kadi yako na paypal sio tatizo, tatizo ni jinsi ya paypal kuihakiki kwamba kweli ni ya kwako.

Paypal wanachofanya ni kukuchaji fedha kidogo (wastani wa 2,000TZS), halafa katika muamala huo wanaweka namba ya siri fulani. Sasa wewe inabidi uangalie statement yako kutoka benki, uione hiyo namba, halafu uwape paypal. Assumption hapo ni kwamba hakuna mtu mwingine anaweza kuona statement yako zaidi ya wewe.

Sasa ndani ya paypal unaweza ukakamilisha taratibu. Ukija CRDB ili kupata tu details za hiyo transaction, jasho litakutoka. Inaweza ukadhani ni kitu simple tu kupata details za transaction (hata mimi nilifikiria hivyo), lakini amini usiamini utashangazwa ... Nimefanya si chini ya trip 10 kwenda CRDB kwa ishu hiii, usihesabu simu, na nimetoka kupiga nyingine sasa hivi ... lol ...

Ningetakiwa niwe nimeshakata tamaa ila tu nataka tu nifuatilie mpaka mwisho waniambie inawezekana au haiwezekani.

Ila kama huu ndio utaratibu, sioni ni jinsi gani wataweza kuwahudumia wateja hata 100 tu wanaotaka kujiunga na paypal. Achilia mbali kwamba hawa watu 100 inabidi wapige kwata CRDB more that 10 times, halafu wawe wanapiga simu mara kwa mara kuwakumbushia CRDB case zao. Na mara nyingi watu unaoongea nao CRDB hata hawaelewi unazungumzia nini.

Makubaliano yako na CRDB ni soo
Ili kuiruhusu kadi yako kutumika online, itabidi utie saini makubaliano yako na CRDB, ambayo yanavipengele ambavyo vinaiondolea CRDB jukumu lolote la kukuhakikishia usalama wako unpotumia kadi yako kwenye mtandao. Kwa hiyo ukiwa online na kadi yako, jua you are on your own.

Kwa watumiaji wengine duniani kuna taratibu za jinsi ya mtu kupinga kuchajiwa transaction ambazo hujazifanya wewe. Na kuna taratibu za jinsi gani utarudishiwa pesa zako.

Mpkataba wa CRDB hauoneshi kama kuna kitu kama hicho. Kwa hiyo mtu akipata details za kadi yako, siku zote itakuwa inakula upande wako.

Kwa hiyo baada ya kuutia saini tu nimehakikisha kadi yangu haiondoki machoni pangu, na pia nahakikisha akaunti hiyo ya CRDB haina vijisenti vingi ... mpaka ntakapomaliza hii exercise.

Hitimisho
Sasa hivi unaweza kutumia kadi yako ya CRDB kwenye mtandao, lakini you do it at your own risk, tena risk kubwa tu.

Kinachonitisha ni kwamba kama kadi yako imewezeshwa kutumika kwenye internet, mtu hana haja ya kukuibia kadi nzima kwa sababu utashtuka, utaripoti, na kadi itafungwa. Anachotakiwa kufanya ni kupata namba za kadi zilizopo mbele, na vile vijinamba vitatu vilivyopo nyuma ya kadi, na inakula upande wako kimya kimya.

Kama umeiwezesha kadi yako kutumika kwenye mtandao, na kama vijinsenti vyako kwenye akaunti yako sio vidogo, na kama huwezi kuitunza details za kadi kiasi hicho, ni vyema ungewaambia waizibe isitumike kwenye mtandao ... or u may have to learn the hard way.
__________________
There are only 10 types of people in the world. Those that understand binary, and those that don't.

Manitoba
Senior Member
Points: 108,272, Level: 100 Points: 108,272, Level: 100 Points: 108,272, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
Join Date: Tue Jul 2008
Posts: 244
Thanks: 17
Thanked 10 Times in 7 Posts
Views: 4888
Reply With Quote
  #11  
Old 19th January 2009, 05:52 PM
Outlier's Avatar
Outlier Outlier is offline
Outlier has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 102,925, Level: 100 Points: 102,925, Level: 100 Points: 102,925, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Sun Dec 2008
Location: somewhere on earth
Posts: 304
Thanks: 1
Thanked 2 Times in 2 Posts
Rep Power: 22
Outlier will become famous soon enoughOutlier will become famous soon enoughOutlier will become famous soon enoughOutlier will become famous soon enoughOutlier will become famous soon enoughOutlier will become famous soon enoughOutlier will become famous soon enoughOutlier will become famous soon enough
Default Re: CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao

Mimi nimetumia huduma hii kwa miezi sita na mpaka sasa sijapata matatizo na ukweli inarahisisha sana transactions zako. Zaidi ya kununua, unaweza pia ku-transfer pesa kwenda kwa mtu mwingine.
Cha muhimu angalau ukumbuke kila siku kuingia mtandaoni na kuangalia salio lako.
Mwanzo mgumu ila am confident "we" are progressing.
Reply With Quote
  #12  
Old 19th January 2009, 06:04 PM
Shadow's Avatar
Shadow Shadow is online now
Shadow arround the World
JF Senior Expert Member
Points: 575,587, Level: 100 Points: 575,587, Level: 100 Points: 575,587, Level: 100
Activity: 13% Activity: 13% Activity: 13%
 
Join Date: Mon May 2008
Posts: 1,175
Thanks: 52
Thanked 113 Times in 65 Posts
Rep Power: 24
Shadow will become famous soon enoughShadow will become famous soon enoughShadow will become famous soon enoughShadow will become famous soon enoughShadow will become famous soon enoughShadow will become famous soon enoughShadow will become famous soon enoughShadow will become famous soon enough
Default Re: CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao

Je kuna haja ya kuomba ushauri wa baraza la walaji? hii ndio kazi yao kumlinda mlaji. Mimi naona kuna haja ya kushirikisha baraza hili na si kukaa kimya.
Reply With Quote
  #13  
Old 19th January 2009, 08:25 PM
Hofstede Hofstede is online now
Hofstede has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 237,341, Level: 100 Points: 237,341, Level: 100 Points: 237,341, Level: 100
Activity: 9% Activity: 9% Activity: 9%
 
Join Date: Sun Jul 2007
Posts: 1,377
Thanks: 197
Thanked 230 Times in 116 Posts
Rep Power: 25
Hofstede will become famous soon enoughHofstede will become famous soon enoughHofstede will become famous soon enoughHofstede will become famous soon enoughHofstede will become famous soon enoughHofstede will become famous soon enoughHofstede will become famous soon enoughHofstede will become famous soon enough
Default Re: CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao

Quote:
View Post
Mimi nimetumia huduma hii kwa miezi sita na mpaka sasa sijapata matatizo na ukweli inarahisisha sana transactions zako. Zaidi ya kununua, unaweza pia ku-transfer pesa kwenda kwa mtu mwingine.
Cha muhimu angalau ukumbuke kila siku kuingia mtandaoni na kuangalia salio lako.
Mwanzo mgumu ila am confident "we" are progressing.
Kwa hili CRDB wamepiga hatua, ila nafikiri cost ya hii kitu itakuwa ni kubwa zaidi ya Benefit. Cha kufanya kwa wale wenye kutaka huduma hii ni bora kuwa na account mbili yaani Moja ni kwa ajili ya transaction za online, unahamisha pesa na kufanya transactions on spot, hapo hapo. Nyingine ni kuhifadhia pesa kama una wasiwasi
Reply With Quote
  #14  
Old 19th January 2009, 08:50 PM
Mtu wa Kawaida Mtu wa Kawaida is offline
Mtu wa Kawaida has no status.
JF Premium Member
Points: 78,284, Level: 100 Points: 78,284, Level: 100 Points: 78,284, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Fri May 2008
Posts: 182
Thanks: 1
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 22
Mtu wa Kawaida will become famous soon enoughMtu wa Kawaida will become famous soon enoughMtu wa Kawaida will become famous soon enoughMtu wa Kawaida will become famous soon enoughMtu wa Kawaida will become famous soon enoughMtu wa Kawaida will become famous soon enoughMtu wa Kawaida will become famous soon enoughMtu wa Kawaida will become famous soon enough
Default Re: CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao

Quote:
View Post

Cha kufanya kwa wale wenye kutaka huduma hii ni bora kuwa na account mbili yaani Moja ni kwa ajili ya transaction za online, unahamisha pesa na kufanya transactions on spot, hapo hapo. Nyingine ni kuhifadhia pesa kama una wasiwasi
Ni kweli kabisa. Hii itaondoa wasiwasi wa kwamba unaibiwa au watu wanachezea account yako.
Reply With Quote
  #15  
Old 19th January 2009, 09:06 PM
Kana-Ka-Nsungu's Avatar
Kana-Ka-Nsungu Kana-Ka-Nsungu is offline
Kana-Ka-Nsungu has no status.
JF Premium Member
Points: 566,991, Level: 100 Points: 566,991, Level: 100 Points: 566,991, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Thu Oct 2007
Location: 10 Dawning Street
Posts: 1,795
Thanks: 8
Thanked 44 Times in 28 Posts
Rep Power: 26
Kana-Ka-Nsungu will become famous soon enoughKana-Ka-Nsungu will become famous soon enoughKana-Ka-Nsungu will become famous soon enoughKana-Ka-Nsungu will become famous soon enoughKana-Ka-Nsungu will become famous soon enoughKana-Ka-Nsungu will become famous soon enoughKana-Ka-Nsungu will become famous soon enoughKana-Ka-Nsungu will become famous soon enough
Default Re: CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao

Sielewi kwa nini CRDB wameifinya hiyo feature ya address, kwa kufanya hivi wenye account zetu tumekuwa more exposed to fraud. Au ndio wanataka kuutangazia ulimwengu mzima kuwa- watanzania hatuna address?
Nisingemshauri mtu yoyote kutumia hii huduma for the time being hadi pale kutakapokuwa na uhakika kwamba kuna 100% protection kwa wateja na Bank iko tayari kuwa responsible pale ambapo kutatokea 'ufisadi'.
__________________
If someone knocks you down- its their faulty, but if you stay down its your faulty.
Reply With Quote
  #16  
Old 20th January 2009, 09:03 AM
Mwanjelwa Mwanjelwa is online now
Mwanjelwa Msema kweli kulingana na muda uliopo.
JF Senior Expert Member
Points: 136,339, Level: 100 Points: 136,339, Level: 100 Points: 136,339, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Sun Jul 2007
Location: Chenorbly
Posts: 520
Thanks: 17
Thanked 25 Times in 17 Posts
Rep Power: 24
Mwanjelwa will become famous soon enoughMwanjelwa will become famous soon enoughMwanjelwa will become famous soon enoughMwanjelwa will become famous soon enoughMwanjelwa will become famous soon enoughMwanjelwa will become famous soon enoughMwanjelwa will become famous soon enoughMwanjelwa will become famous soon enough
Default Re: CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao

[QUOTE=Manitoba;360386]Mzee mimi nadhani wanao-design hizi technologies huwa wanashirikisha sana akili. Kama tungekuwa sisi basi ndio tungesema hivyo kirahisi tu kwamba "Inaweza kukubamiza au kukunyanyua".

Nakubaliana nawe. Ninaposema inaweza kukubamiza kwa mfano wa hizi Crdit Cards, ni pale ambapo unaweza ibiwa! Wanaibiwa wengi sana duniani. Ila lengo lake ni kurahisisha mambo kama ilivyo.


Tofauti ya CRDB card hapa nikwamba mtu akitumia card yako ya CRDB, na ukaona transaction ambayo hukuifanya wewe, huna pa kulalamika. Maana yake CRDB ni kama wanasema ukiibiwa ni shauri yako. Yaani inawezekana hata kumtafuta mwizi wasikusaidie. Wakati kwa wenzetu ukiibiwa aliyesaidia wizi ndio anabanwa.


Mimi hapo sioni tofauti. Kwani katika mazingira yote uliyoweka, hakuna sehemu ambayo Insuarer wa CC yako anawajibika kukulipa (compensation). Every transaction done is at your own risk.Nadhani unafahamu kwanini licha ya Bank kukupatia ATM Card wewe, wenyewe kama Bank huwa hawatakiwi kuijua na hawawezi? Suala la kubanwa kama unvyoliongelea ni la kawaida, unaweza pata pesa yako au usipate!. Naongelea losses hapa.

Naamini CRDB iko sawa sawa na tutafika kule wengine waliko. Mtoto asipochafuka unadhani atajuaje kucheza mpira wa miguu?
Reply With Quote
  #17  
Old 20th January 2009, 04:09 PM
Manitoba Manitoba is offline
Manitoba has no status.
Senior Member
Points: 108,272, Level: 100 Points: 108,272, Level: 100 Points: 108,272, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Tue Jul 2008
Posts: 244
Thanks: 17
Thanked 10 Times in 7 Posts
Rep Power: 22
Manitoba will become famous soon enoughManitoba will become famous soon enoughManitoba will become famous soon enoughManitoba will become famous soon enoughManitoba will become famous soon enoughManitoba will become famous soon enoughManitoba will become famous soon enoughManitoba will become famous soon enough
Default Re: CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao

Quote:
View Post
Mimi nimetumia huduma hii kwa miezi sita na mpaka sasa sijapata matatizo na ukweli inarahisisha sana transactions zako. Zaidi ya kununua, unaweza pia ku-transfer pesa kwenda kwa mtu mwingine.
Cha muhimu angalau ukumbuke kila siku kuingia mtandaoni na kuangalia salio lako.
Mwanzo mgumu ila am confident "we" are progressing.
Sawa kaka.

Sisemi kwamba wewe ndio ulivyo, ila sisi tuna kawaida sana ya zima moto. Kwa sababu inafanya kazi, basi kheri. Yakianza kutokea matatizo, unaona kama muujiza na kulalama kwa nini benki yako haikulindi. Lakini pengine mtu ungejua ukweli ulivyo, mtu ungejua risks ziko wapi na ungekuwa makini zaidi na unachokifanya.

Quote:
View Post
Sielewi kwa nini CRDB wameifinya hiyo feature ya address, kwa kufanya hivi wenye account zetu tumekuwa more exposed to fraud. Au ndio wanataka kuutangazia ulimwengu mzima kuwa- watanzania hatuna address?
Nisingemshauri mtu yoyote kutumia hii huduma for the time being hadi pale kutakapokuwa na uhakika kwamba kuna 100% protection kwa wateja na Bank iko tayari kuwa responsible pale ambapo kutatokea 'ufisadi'.
Sadakta! Ndio maana nikasema, "usithubutu ila tu kama unajua unachokifanya".

Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba kwa jinsi CRDB wanavyoitangaza kama vile hakuna risk yoyote, watu watazikurupukia na wengi wataumia.

Bottom line is, know what you are doing.

[QUOTE=mwanjelwa;360746]
Quote:
View Post
Mzee mimi nadhani wanao-design hizi technologies huwa wanashirikisha sana akili. Kama tungekuwa sisi basi ndio tungesema hivyo kirahisi tu kwamba "Inaweza kukubamiza au kukunyanyua".

Nakubaliana nawe. Ninaposema inaweza kukubamiza kwa mfano wa hizi Crdit Cards, ni pale ambapo unaweza ibiwa! Wanaibiwa wengi sana duniani. Ila lengo lake ni kurahisisha mambo kama ilivyo.


Tofauti ya CRDB card hapa nikwamba mtu akitumia card yako ya CRDB, na ukaona transaction ambayo hukuifanya wewe, huna pa kulalamika. Maana yake CRDB ni kama wanasema ukiibiwa ni shauri yako. Yaani inawezekana hata kumtafuta mwizi wasikusaidie. Wakati kwa wenzetu ukiibiwa aliyesaidia wizi ndio anabanwa.


Mimi hapo sioni tofauti. Kwani katika mazingira yote uliyoweka, hakuna sehemu ambayo Insuarer wa CC yako anawajibika kukulipa (compensation). Every transaction done is at your own risk.Nadhani unafahamu kwanini licha ya Bank kukupatia ATM Card wewe, wenyewe kama Bank huwa hawatakiwi kuijua na hawawezi? Suala la kubanwa kama unvyoliongelea ni la kawaida, unaweza pata pesa yako au usipate!. Naongelea losses hapa.

Naamini CRDB iko sawa sawa na tutafika kule wengine waliko. Mtoto asipochafuka unadhani atajuaje kucheza mpira wa miguu?
Kweli huoni tofauti? Umeshasikia kitu kinaitwa "Charge Back"? Kama hujawahi basi ndio maana huoni tofauti.
Soma kidogo hapa: Chargeback - Wikipedia, the free encyclopedia

Ukweli ni kwamba kwa wenzetu interest za mwenye kadi zinalindwa, wakati hapa CRDB imejitoa jukumu lolote la kufanya hivyo. Yaani kwa CRDB kukiwa na transaction ya makosa au fraudulent transaction, basi ndio umeuwawa. Kwa wenzetu kunakuwa na taratibu za jinsi gani ya ku-complain, na hata kurudishiwa pesa zako. Kwa CRDB hakuna, kama huamni kasome kale kamkataba. "Every transaction done is at your own risk" ni statement inayoweza kutolewa na CRDB na issuer wengine wasiojali maslahi ya mwenye kadi kabisa.

Mzee bado huoni tofauti?

Kweli kufika tutafika. Lakini wakiendelea kuwa na customers wanaokubali wasiwe na rights namna hiyo kila kitu namna hiyo, basi twawezafika tukiwa tumechelewa kiaina.

Ngoja labda nikupe sababu kwa nini wenzetu wanaona kuna umuhimu wa kuweka kitu kama "Charge Back" tena mpaka kwenye sheria zao.

Mantiki sio tu kumlinda mtu na pesa zake tu. Ni kwamba usipoweza kuwa-assure watu kwamba they are safe, in the long run wengi wata-opt-out. Na ukiwa na wengi hawaingiii kwenye hiyo system, ndio tutakuwa tunachelewa hivyo kufika.

Halafu pia kuwepo kwa "Charge Back" kunamfanya mtoa huduma kuchukua steps kuhakikisha kwamba CC/DB ni halali, na pengine mtumiaji ni halali. Hizi steps zipo tayari, na watu wanazitumia. Ukiondoa "Charge Back", mtoa huduma hatakuwa na incentive yoyote kuhakiki kwamba matumizi ya CC/DB ni halali.

Kama huelewi hilo wewe subiri pale makampuni ya ki-tz yatakapo anza kutoa huduma online, na kucharge kwa kutumia hiyo Visa card ya CRDB. Naweza nikakwambia kitakachotokea. Either watu hawatatumia hizo huduma, ama CRDB watabadili hako kamkataba.

Kuna mzee wangu mmoja aliniambia kuona mbele si kazi, hata mbuzi anaona mbele. Kuona mbali ni issue.

<rant>
Pengine tujitahidi kuepuka kuweka statement za jumla jumla ambazo hatuna uhakika nazo, ili mradi tu kusupport argument zatu.
Unapoweka statement kama "hakuna sehemu ambayo Insuarer wa CC yako anawajibika kukulipa (compensation)", halafu kukakosekana mtu wa kuonyesha kwamba umekosea, unakuwa umepotosha wengi baba.
</rant>
__________________
There are only 10 types of people in the world. Those that understand binary, and those that don't.

Last edited by Manitoba; 20th January 2009 at 04:46 PM..
Reply With Quote
  #18  
Old 20th January 2009, 05:47 PM
Mwanjelwa Mwanjelwa is online now
Mwanjelwa Msema kweli kulingana na muda uliopo.
JF Senior Expert Member
Points: 136,339, Level: 100 Points: 136,339, Level: 100 Points: 136,339, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Sun Jul 2007
Location: Chenorbly
Posts: 520
Thanks: 17
Thanked 25 Times in 17 Posts
Rep Power: 24
Mwanjelwa will become famous soon enoughMwanjelwa will become famous soon enoughMwanjelwa will become famous soon enoughMwanjelwa will become famous soon enoughMwanjelwa will become famous soon enoughMwanjelwa will become famous soon enoughMwanjelwa will become famous soon enoughMwanjelwa will become famous soon enough
Default Re: CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao

[QUOTE=Manitoba;361068]
Pengine tujitahidi kuepuka kuweka statement za jumla jumla ambazo hatuna uhakika nazo, ili mradi tu kusupport argument zatu.
Unapoweka statement kama "hakuna sehemu ambayo Insuarer wa CC yako anawajibika kukulipa (compensation)", halafu kukakosekana mtu wa kuonyesha kwamba umekosea, unakuwa umepotosha wengi baba.



Mkuu, inaonyesha wewe umesome tu kwenye shule kuhusu credit cards. Mimi siyo mtalaamu wa uchumi wala mtu wa banki, ila nimetumia CC kadhaa. Labda siwezi kueleza zaidi kwa sababu hiyo. Ila kuhusu wizi kwa credits cards na compensation unaweza check hapa upate info zaidi ya ile niliyokupatia. <http://en.wikipedia.org/wiki/Credit_card_fraud>
Huyu jamaa pamoja na huyu <http://www.securityfocus.com/news/11493> wanakuambia kuwa ni hela nyingi sana zinaibiwa Duniani kwa CC kila mwaka. Hao wote si CRDB. SOma kwa makini sana.


Hatubishani ila tunaongelea kwa uzoefu wa kutumia na si kusoma shule na pia kupeana ujumbe kwa kutumia experience. Siwateti CRDB kwa namna yoyote ile na CRDB hawawezi kufanana na Inter-national companies za America au Europe za CC. Pia pamoja na kuwa kuna hiyo disclamer kwa CRDB nimewahi fanya makosa ya k-transaction kwa tune ya equivalent ya 500,000TSHS. Nili-report international Banking section pale CRDB TZ wakarekebisha in three days.

Ila ninasema kwamba wako sawa sawa kulingana u-TZ kule. Wata-improve tu service zao with time. Sio muda wa kuanza kwaponda kuwa wao nyuma na hawajali rights za wateja wao. Kuna banks kadhaa za SEA zina masharti magumu sana na nilishangaa sana jinsi wateja wanavyo-chargiwa services a hizo benks ukifananisha na Europe au TZ na jinsi wanavyolalamika sana. Lakini bankers wana sababu.

Tujitahidi kupenda home na vitu vya home. Vilivyo majuu havikushuka. Vilianza hivi hivi.

Take home message: Shule ina umuhimu wake. Ila uzoefu wa siku nyingi una umuhimu zaidi. Rubani aliyekuwa trained kuendesha Boeings za abiria mwaka jana, hawezi kuanza na 747-400 immediately. Lazima aanzie chini kwenye 737-200 kwanza!
Reply With Quote
  #19  
Old 20th January 2009, 05:55 PM
Caroline Danzi Caroline Danzi is offline
Caroline Danzi online
JF Senior Expert Member
Points: 75,195, Level: 100 Points: 75,195, Level: 100 Points: 75,195, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Fri Dec 2008
Location: Dar es Salaam
Posts: 456
Thanks: 2
Thanked 51 Times in 38 Posts
Rep Power: 22
Caroline Danzi will become famous soon enoughCaroline Danzi will become famous soon enoughCaroline Danzi will become famous soon enoughCaroline Danzi will become famous soon enoughCaroline Danzi will become famous soon enoughCaroline Danzi will become famous soon enoughCaroline Danzi will become famous soon enoughCaroline Danzi will become famous soon enough
Default Re: CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao

Tehe tehe sisi wa vijijini tumepona maaan tumezoea kupanga foleni ya NMB, VISA wapi na wapi? Asante kwa taarifa incase tumepata na sisi fulsa hiyo tutakuwa makini.
Reply With Quote
  #20  
Old 20th January 2009, 08:46 PM
Kinvaba Kinvaba is offline
Kinvaba a man of truth
Senior Member
Points: 76,366, Level: 100 Points: 76,366, Level: 100 Points: 76,366, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Mon Feb 2008
Location: ubaruku
Posts: 120
Thanks: 0
Thanked 1 Time in 1 Post
Rep Power: 23
Kinvaba will become famous soon enoughKinvaba will become famous soon enoughKinvaba will become famous soon enoughKinvaba will become famous soon enoughKinvaba will become famous soon enoughKinvaba will become famous soon enoughKinvaba will become famous soon enoughKinvaba will become famous soon enough
Default Re: CRDB Visa Card: Usithubutu kuitumia kwenye Mtandao

Nakushukuru sana Manitoba. Wahenga walisema, ukiona mwenzio ananyolewa, nawe tia maji. Kinga ni bora kuliko kutibu. Nawashauri wenzangu wote tunaotumia kadi hii ya CRDB tuwe makini, tusipuuzie kwani kilio kitakuwa mjukuu wetu. CRDB nao wanatakiwa kujibu maswali wanayoulizwa na wateja wao kuhusu usalama wa matumizi ya kadi hii, kwani kukaa kimya nako kunatoa mwanya kwa wateja wao na watu wengine kusema wanayoona yanawafaa
__________________
Mwana wa Msakuzi
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
card, crdb, kuitumia, kwenye, matumizi, mtandao, mtandaoni, usithubutu, utata, visa, yake


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On


Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
BoT Scandal: Tulikotoka, Tulipo, Tunakoelekea Maxence Melo Jamii Intelligence 3079 12th November 2009 08:12 AM
Muafaka CCM na CUF, pande mbili za shilingi! MwanaCCM Jukwaa la Siasa 148 13th July 2009 10:13 AM
Hotuba Mbadala TAMISEMI: Slaa ataka Balali ajiuzulu; ambana Lowassa kuhusu Richmond John Mnyika Jukwaa la Siasa 13 16th December 2008 02:21 PM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 03:02 PM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com