Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar

    Report Post
    Page 3 of 5 FirstFirst 12345 LastLast
    Results 41 to 60 of 89
    1. #1
      Mgumu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd November 2006
      Posts : 237
      Rep Power : 689
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar

      Kwa wakazi wa Dar na vitongoji nyake taarifa hii ni kukatisha tamaa, kutokana na usumbufu ninaupata kila asubuhi na jioni kugombania dalala nathubutu kusema hatuna serikali na kama ipo imekwenda likizo.

      Hivi ile pesa ya Richmond,IPTL au rada ingewekezwa kwenye miradi ya usafiri hapa nchini, tungekuwa mbali.

      Mungu yupo hawa mafethuli siku zao zinahesabika


      Mradi wa mabasi yaendayo kasi ni kitendawili kigumu

      Mobini Sarya

      KAMA kuna kitu ambacho wakazi wa Dar es Salaam, walikuwa wanakisubiri kwa hamu na kwa muda mrefu, ni mradi wa usafiri mpya wa mabasi yaendayo kasi, uliotarajia kuanza mapema mwaka huu.

      Usafiri jijini Dar es Salaam, ambako asilimia saba ya Watanzania wanaishi wakisaka maisha, unatajwa kuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi.

      Kutokana na kukosekana usafiri wa uhakika katika jiji hili, inakisiwa kuwa, wakazi wake hupoteza wastani wa saa zaidi ya tatu kwa siku nje ya ofisi zao.

      Pia inakisiwa kuwa, asilimia 70 ya pato la taifa, huzalishwa kwenye jiji hili, lakini pamoja na umuhimu huo, mapato yanayopatikana yameshindwa kutumiwa vyema kuboresha miundombinu ikiwamo barabara ambazo nyingi ni zile zilizojengwa wakati wa uhuru.

      Tatizo la usafiri Dar es Salaam, kushindwa kutatuliwa na mamlaka zinazohusika, ni kielelezo tosha cha uwajibikaji hafifu kwa baadhi ya watendaji, hasa katika maeneo fulani yaliyobinafsishwa. Kwa mfano tangu serikali ilipojitoa kwenye sekta ya usafiri jijini Dar es Salaam na kuamua kuikabidhi Kampuni ya Usafiri jijini humo (UDA) kwenye sekta binafsi, kampuni hiyo imeshindwa kuleta matumaini.

      Hadi sasa, inakisiwa kuwa wastani wa abiria 123,000 hutumia usafiri wa daladala, ambazo zinakadiriwa kufikia 9,300, zinazotoa huduma kwa siku, huku ikikadariwa kuwa, abiria zaidi ya 100,000 hukosa usafiri huo. Aidha, husafiri kwa miguu, baiskeli, pikipiki, gari ndogo na hata kupanda malori ya mizigo.

      Katika uchunguzi uliofanywa mwaka 2004, ilibainika kuwa kila siku daladala moja hupoteza sh 6,000 sawa na sh 180,000 kwa mwezi, ambazo hutumika kuwalipa wapiga debe.

      Pesa hizo kama zingekusanywa na Chama cha Wamiliki wa Daladala (TABOA), kwa daladala 9,300, wangepata zaidi ya sh milioni 55 kwa mwaka.

      Pesa hizo zingeunda kampuni ya usafirishaji jijini (KAUJI) na wengeweza kuzitumia kama dhamana kupata mkopo ili kuagiza mabasi mengi makubwa.

      Kutokana na umuhimu huu wa usafiri wa jiji, serikali imekuwa ikilaumiwa kwa kushindwa kuuoboresha kwa kupanua miundombinu ili watu wawe wanawahi kazini na wanafunzi wanawahi mashuleni ili taifa lipate maendeleo.

      Ndio maana Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, ikaamua kubuni na kutangaza kuanzisha mradi wa usafiri wa mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam (Dar Rapid Trans - DART), ambao kila mara wamekuwa wakiwatangazia wananchi kuwa ungeanza mapema mwaka huu.

      Wananchi wanashangaa na wanashindwa kupata majibu kamili, ilikuwaje taarifa zilikuwa zikitolewa na kuwapa watu matumaini, wakati mradi huo ambao unasubiriwa na wengi haujawa tayari? Taarifa hizo zilianza Agosti mwaka jana, kwamba mradi huo wa DART ungeanza kutoa huduma, lakini haikuwa hivyo.

      Mradi huo, unasimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, mwishoni mwa waka jana ilitolewa taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa, mradi huo ungeweza kuanza kazi Machi, mwaka huu. Wananchi wakazidi kuvuta subira, hasa wale wa Mabagala na Gongo la Mboto, ambao usafiri mzuri kwao ni anasa na kupita kwenye madirisha ya mabasi wala si jambo la kushangaza.

      Taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa, inaonekana kuwa usafiri huo utakuwa wa usalama, uhakika na wa haraka hali inayowapa matumaini makubwa wakazi wa Dar es Salaam.

      Wakati tulipokuwa tukiambiwa mradi unaanza mwezi wa Agosti, mara mwaka kesho, ulikuwa ni wimbo mtamu ambao msikilizaji alikuwa hauelewi vema. Aidha, mwimbaji alikuwa anatumia ujanja kumliwaza msikilizaji hata kama wimbo huo ulikuwa unaimbwa kwa mafumbo.

      Wanasema kuwa, unaweza kuwadanganya watu wote, lakini si kwa wakati wote, huo msemo ndio ulinifanya nikapiga hodi kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam ili nifahamu ukweli wa mradi huu kwamba utaanza lini.

      Nilipofika kwenye ofisi hiyo, haikuwa kazi rahisi kupata taarifa, kwani ofisa niliyekutana naye kwenye ofisi za kitengo hicho, hakuwa tayari kutoa ukweli huo na hata habari hizo hazikumfurahisha, baada ya kufahamu kuwa nilikuwa nataka kujua ni lini usafiri huo utaanza rasmi.

      Baada ya mabishano ya muda mrefu, hatimaye tulifikia mwafaka na akanipeleka kwa ofisa mwingine aliyeniahidi kuwa, nirudi baada ya mwaka mpya ili aweze kunipatia taarifa kamili, sikufanya ubishi, niliondoka na mwaka mpya ulipoanza nilikwenda tena kwenye ofisi hizo.

      Wakati najaribu kufuatilia habari hii, kichwani nilikuwa najiuliza habari ya mradi mwingine wa kuzalisha umeme, uliokabidhiwa kampuni moja ya nje yenye jina la Richmond, ambao wasemaji wake walikuwa wakipiga danadana tarehe ya uhakika ya kuanza kuzalisha umeme.

      Baada ya kufika, nilikabidhiwa ripoti kamili iliyoandaliwa Desemba 5, mwaka jana kutokana na kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Manispaa ya Temeke na kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam, wadau pamoja na mkuu wa mkoa.

      Kwenye mkutano huo, ambao walialikwa pia waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro, akitoa hotuba yake alisema miundombinu kwa ajili ya mradi huo inatarajiwa kuanza mwaka huu, na huduma ya usafiri itaanza kutolewa rasmi mwaka 2009, kisha akamaliza kwa kusema “hatutarajii mipango isiyo na mwisho, tunataka matokeo.”

      Lakini pamoja na taarifa hiyo kubainishwa kwamba usafiri utaanza rasmi mwaka 2009, taarifa ambazo zilitoka kwenye vyombo vya habari, zilikuwa zinabainisha kuwa, huduma hii ya usafiri wa mabasi yaendayo kwa kasi itaanza Machi mwaka huu.

      Taarifa kwenye vyombo hivyo zilisisitiza pia kuwa, hata daladala ndogo zitapigwa marufuku kuingia katikati ya jiji, baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wameagiza magari hayo, waliingiwa na hofu na hata wengine wakarudisha magari waliyokuwa wameagiza kwa hofu kuwa huenda yangeshindwa kufanya kazi. Hakuna lililoendelea, mambo hayo ni sawa na tunda bichi ambalo halijawa tayari kuliwa.

      Ukweli ni kwamba, kama kuna wafanyabiashara waliokuwa wamesita kuagiza magari ya kutolea huduma, ni bora wakabadilisha msimamo wao na kuagiza magari hayo, kwani ukweli ni kuwa, mradi huo unaelezwa kuwa, unatarajiwa kuanza kutoa huduma kuanzia Machi 30 mwaka 2009 kwa kutumia mabasi yenye uwezo wa kubeba abiria 140 na 160, tena kwa kuanzia katika Barabara ya Morogoro tu.

      Mpango mzima wa mradi huo na ambao labda unaweza kumaliza tatizo la usafiri jijini, unatarajiwa kukamilika mwaka 2035, kutokana na mpango huo kugawanywa katika awamu sita, ambazo zina jumla ya kilometa 137, ambazo barabara na miundombinu mingine itakuwa ikitengezwa kwa awamu.

      Kutokana na ripoti hiyo, inaonekana kuwa, kuanzia Machi 2007 wataalamu wa mradi huo wataanza kusanifu barabara zenye kilometa 20.9 ambazo zitahusisha vituo vya Kimara, Ubungo, Morocco, Kariakoo na Kivukoni katika zoezi hilo litakalokwenda sambamba na kufanyia tathmini wale wote wanaopaswa kulipwa fidia ya kuhamishwa ili kupisha ujenzi wa barabara mpya, ambazo zitatumiwa na mabasi hayo.

      Shughuli hii inatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu na ujenzi wa awamu ya kwanza ya mradi unatarajiwa kugharimu sh bilioni 122, ambazo zinatolewa na Benki ya Dunia na watakaoshughulika na ujenzi huo ni Wakala wa Barabara nchini (TANROADS).

      Awamu hiyo ya kwanza ya mradi itakuwa na barabara yenye urefu wa km. 20.9 na itakuwa imegawanyika katika sehemu kuu tano, ambazo ni zile za wanaokwenda kwa miguu, baiskeli, magari ya watu binafsi vituo vya daladala nyingine na vile vya mabasi hayo maalumu.

      Nauli ambazo zinapendekezwa mradi huu ukikamilika ni kati ya sh 200 na 300 hadi 500 mpaka mwisho wa safari.

      Tathimini iliyofanywa mwaka 2004, ilibainika kuwa, Barabara ya Morogoro inaongoza kwa kupitiwa na magari mengi na ndipo mradi utakapoanzia na baada ya hapo itafuatia Barabara ya Kilwa ambayo nayo inatumiwa zaidi. Mradi wa awamu ya pili utakaohusisha barabara hiyo utaanza mwaka 2012 ukiwa na kilometa 19.3 na awamu ya tatu itakuwa mwaka 2016 ukiwa na barabara ya km. 23.6.

      Awamu ya sita na ya mwisho inatarajiwa kukamilika mwaka 2035 takribani miaka 10 baadaye, kama mipango itakwenda kama inavyoelezewa na kama yatazingatiwa maneno ya Kandoro aliyosema kwa ‘hatutarajii kuwa na mipango isiyo na mwisho’, lakini vilevile itategemea sera ya viongozi wanaofuata miaka kumi inayokuja.

      Kwa hali yoyote ile, kukamilika kwa mradi huu ni sawa na mwenye njaa anayesubiri matunda yaive ndipo ale, kama mradi huu unategemea fedha za wafadhili ndio utekelezwe, matumaini yake ni madogo, na hata kama ni wawekezaji, basi wasiwe na sura ya Richmond, ambao wataendeleza yale ya ngoja leo ngoja kesho.

      Kulingana na maelezo ya mradi huu unaotarajiwa kukamilika mwaka 2035, amabako wengi hatutarajiwi kuwapo hai, tungeomba serikali itazame njia haraka na mbadala kama ya usafiri wa baharini na kuingia ubia na mwekezaji mpya wa TRC ili aweke usafiri wa reli kupita maeneo ya jiji ili kuondoa adha kwa wananchi.

      Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa anwani ya: barua pepe; [email protected]. Simu; 0753 399 579 au 0717 328 102.
      Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili

    2. Miaka 50

    3. #41
      kimatire's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2008
      Location : Sydine- St. Roix's
      Posts : 349
      Rep Power : 608
      Likes Received
      43
      Likes Given
      20

      Default Re: Mradi wa Mabasi ya Kasi wapigwa Kalenda

      Yapo mambo ya kitaalamu yanahitajika kufanywa kwa umakini wa hali ya juu ili mradi wa jinsi hii uweze kuanza kazi.Moja wapo ni hilo la ujenzi wa Miundo mbinu jingine ni la upatikanaji wa magari hayo, na la tatu ni mfumo wa uongozaji na ukusanyaji wa nauli.Kwa wale waliobahatika kwenda katika nchi za Brazil,Chile,China,Cleverland( USA) watakubaliana nami kuwa kuna kazi kubwa inayotakiwa kufanyika ili mfumo huu wa mabasi yaendayo haraka uweze kufanya kazi katika jiji letu.
      Lakini kwa akili ya mtu wa kawaida hawezi kulielewa hili kwa mapana yake ,kwani anakuwa ana ulinganisho na mabasi tu makubwa au Ikarius,Kumbe ni mfumo mwingine kabisa wa usafiri wa haraka wa kisasa na wenye kuhitaji teknolojia ya GPS na GSM Kuuendesha.Hivyo tuwape nafasi wataalam wenye fani zao wafanye kazi kwa uhakika huku tukitarajia huduma bora kwa siku za usoni kama miaka mitatu hivi kuanzia sasa.Binafsi naujua mfumo huo ambao unajulikana kama BRT-Bus Rapid Transit Systems.Umeanzia chi za Latin America na kusambaa Mashariki ya mbali, na sasa ndo unaingia Afrika ukiwa umetekelezwa huko Lagos Nigeria, Afrika ya Kusini kwa ajili ya kombe la dunia na sasa ndo umebisha hodi hapa kwetu Bongo.Tuwe na imani na subira tutafika siku ya siku, siyo blaaah blaah wala maneno ya kisiasa bali ni kweli tupu kwamba kazi ni kubwa sana.Inahitaji umakini wa hali ya juu sanaa.
      I smile because I don't know what the hell is going on.

    4. #42
      Mkaa Mweupe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th June 2007
      Posts : 581
      Rep Power : 725
      Likes Received
      65
      Likes Given
      4

      Default Re: Mradi wa Mabasi ya Kasi wapigwa Kalenda

      Naomba nitoe angalizo.

      Kwa kawaida ya watanzania tumezoea kuwa mawaziri ndio wazungumzaji wa miradi ilhali waziri kuwepo katika wizara husika kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu sio wa lazima kwa kuwa Rais anaweza kubadili waziri wakati wowote.

      Kwa hali hii inabidi miradi kama hii inapaswa kuwa chini ya katibu wa wizara husika na yeye ndio awe msemaji si hawa wanasiasa.

      Mpoo...
      The best way to get out of dificulty is through it

    5. #43
      mmaroroi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th May 2008
      Posts : 2,181
      Rep Power : 1000
      Likes Received
      104
      Likes Given
      79

      Default Re: Mradi wa Mabasi ya Kasi wapigwa Kalenda

      Mradi huo hautaanza hadi wakubwa wapate pa kupeleka vipanya vyao na kununua hayo mabasi makubwa.Wakubwa wetu hawajali shida ya usafiri iliyopo wanachoangalia wao ni namna gani watakamua fedha nyingi zaidi kwa gharama nafuu.

    6. #44
      JamiiForums's Avatar
      Official Robot Array
      Join Date : 9th November 2006
      Posts : 16,145
      Rep Power : 5882
      Likes Received
      251
      Likes Given
      3

      Default U.S. officials tour Dar Rapid Transport planned facilities

      Attached Thumbnails  

    7. #45
      Koba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd July 2007
      Location : Pasadena California
      Posts : 4,014
      Rep Power : 1410
      Likes Received
      178
      Likes Given
      105

      Default Re: U.S. officials tour Dar Rapid Transport planned facilities

      watafanya kila kitu kuanzia kupiga vipanya marufuku mpaka hiyo DART etc lakini bila kujenga na kuongeza barabara itakuwa ni kujaza maji kwenye gunia tuu!
      "Freedom is incomplete if it is exercised in poverty."-Harry Schwaz

    8. RukaaJuu Final

    9. #46
      Sonara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2008
      Posts : 625
      Rep Power : 668
      Likes Received
      23
      Likes Given
      1

      Default Re: U.S. officials tour Dar Rapid Transport planned facilities

      Madolla yanamwagwa na wamarekani shukrani kwa Rais kikwete safari zake zimezaa matunda kuliko wakati wa Rais yeyote yule aliyewahi kukamata madaraka hapa Tanzania mnajionea wenyewe kazi yake na nema zinavyo miminika kuanzia USA ,Europa, Asia, ni kupeta tu .Hongera Jk

    10. #47
      Mwiba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd October 2007
      Posts : 4,594
      Rep Power : 2085
      Likes Received
      223
      Likes Given
      19

      Default Re: U.S. officials tour Dar Rapid Transport planned facilities

      Hiyo si hongera ya kupewa Kikwete bali hongera ya kupewa wananchi kuwavumilia mafisadi
      Light travels faster than sound. This is why some people appear bright until you hear them speak.

    11. #48
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7663
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: U.S. officials tour Dar Rapid Transport planned facilities

      Lakini Marekani haijulikanai kwa kuwa na Public transit nzuri hata kidogo. Kuna states hazina usafiri mzuri na mipango ya Usafiri nxcchini humo ni tatizo sugu ambalo limewashinda viongozi kibao wa wajimbo..
      Kwa nini serikali yetu isitazame nchi zenye usafiuri mzuri kama vile UK, France, Canada na kadhalika badala ya Marekani?.
      Exploration of reality

    12. #49
      Kwame Nkrumah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd December 2008
      Posts : 857
      Rep Power : 705
      Likes Received
      289
      Likes Given
      294

      Default Re: U.S. officials tour Dar Rapid Transport planned facilities

      Tumeishaanza kupeana hongera hata jiwe la msingi halijawekwa ....!!!!
      I take it personal with Mafisadi.

    13. #50
      Sikonge's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th January 2008
      Location : Sikonge, Tabora
      Posts : 7,858
      Rep Power : 2332
      Likes Received
      2868
      Likes Given
      5532

      Default Re: U.S. officials tour Dar Rapid Transport planned facilities

      Quote By Mkandara
      Lakini Marekani haijulikanai kwa kuwa na Public transit nzuri hata kidogo. Kuna states hazina usafiri mzuri na mipango ya Usafiri nxcchini humo ni tatizo sugu ambalo limewashinda viongozi kibao wa wajimbo..
      Kwa nini serikali yetu isitazame nchi zenye usafiuri mzuri kama vile UK, France, Canada na kadhalika badala ya Marekani?.
      Mkandara umejuaje?

      Nilishawahi kuwaona viongozi wa state moja (Arkansas??) ya USA wakija Europe kuangalia jinsi Public Transport zinavyofanya kazi maana wao hawana. Walitembelea nchi nyingi na kujionea wenyewe mambo yalivyo.

      Hii kitu ni kweli kabisa, miji kama London, Paris, Moscow, Praga, Berlin nk unaweza kujionea mwenyewe jinsi jamaa walivyofanya vitu vyao.
      Ukifika pale Berlin kuna hizi train za chini ya ardhi na juu ya ardhi (S-and U-Bahn), kwa kweli zinabeba watu hadi unashindwa kuamini. Hapo ongeza mabasi kibao juu. Unamalizia kwa matrain yanayokuja Berlin na kwenda pembezoni au miji ya karibu. Ukiachilia hilo, wamejenga rings za highways kuzunguka Berlin. Paris nao wana ring zao.

      Kwa Tanzania nilishaandika sana kuwa pale Dar, bila ya njia za reli, hakuna tutakalofanikiwa. Pia inabidi kuweka kujenga ring nyingine maana Mandela Road kwa sasa imezidiwa mno. Na ikibidi basi waanze kabisa kuplan ya tatu ili mji utakapokuwa, basi tayari iwepo barabara. Hili hata Dodoma, Arusha, Mwanza, Moshi, Mbeya, Mtwara inabidi lianze kufanyika maana hii miji yakua kwa speed kubwa sana.
      Wengine akina yala masikini kama Tabora, Kigoma, Singida nk si vibaya na wao wakaanza kuweka plan zao tayari ili ikitokea BOOM basi wawe wamejiandaa kwa barabara pana katikati ya mji (ikiwezekana 6 lanes).
      Nguruwe pita leo sina Mkuki(By Malila wa JF).

    14. #51
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,261
      Rep Power : 31393
      Likes Received
      9625
      Likes Given
      685

      Default Re: U.S. officials tour Dar Rapid Transport planned facilities

      Quote By Mkandara
      Lakini Marekani haijulikanai kwa kuwa na Public transit nzuri hata kidogo. Kuna states hazina usafiri mzuri na mipango ya Usafiri nxcchini humo ni tatizo sugu ambalo limewashinda viongozi kibao wa wajimbo..
      Kwa nini serikali yetu isitazame nchi zenye usafiuri mzuri kama vile UK, France, Canada na kadhalika badala ya Marekani?.
      True...public transportation kwenye majimbo mengi ya Marekani ni mbofu kweli. Kuna sehemu mtu kama huna gari lako binafsi huwezi hata kuishi.
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    15. #52
      Koba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd July 2007
      Location : Pasadena California
      Posts : 4,014
      Rep Power : 1410
      Likes Received
      178
      Likes Given
      105

      Default Re: U.S. officials tour Dar Rapid Transport planned facilities

      Quote By Nyani Ngabu
      True...public transportation kwenye majimbo mengi ya Marekani ni mbofu kweli. Kuna sehemu mtu kama huna gari lako binafsi huwezi hata kuishi.
      ....ni kweli mheshimiwa Ngabu,washauri wenzako wasihamie huku wakaishia kukimbia kama ulivyokimbia wewe!
      "Freedom is incomplete if it is exercised in poverty."-Harry Schwaz

    16. #53
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,261
      Rep Power : 31393
      Likes Received
      9625
      Likes Given
      685

      Default Re: U.S. officials tour Dar Rapid Transport planned facilities

      Quote By Koba
      ....ni kweli mheshimiwa Ngabu,washauri wenzako wasihamie huku wakaishia kukimbia kama ulivyokimbia wewe!
      Vipi lile demu lako bonge la makaratasi?
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    17. #54
      Bongolander's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Location : Tandale
      Posts : 4,035
      Rep Power : 1418
      Likes Received
      610
      Likes Given
      44

      Default Re: U.S. officials tour Dar Rapid Transport planned facilities

      Quote By Sonara
      Madolla yanamwagwa na wamarekani shukrani kwa Rais kikwete safari zake zimezaa matunda kuliko wakati wa Rais yeyote yule aliyewahi kukamata madaraka hapa Tanzania mnajionea wenyewe kazi yake na nema zinavyo miminika kuanzia USA ,Europa, Asia, ni kupeta tu .Hongera Jk
      Mkuu Tatizo la Tanzania sio fedha, fedha zipo tatizo ni mismanagement ya fedha na matumizi mabaya ya fedha. Kibaya zaidi ni mismanagement ya miradi yeneywe. Hii BRT ikikaa muda mrefu sana ni miaka mitano tu. Unless waachwe watakaojenga wamanage mpaka mwisho.

      NDIVYO TULIVYO- Tunataka pesa tu, hata kama tunazo tunapenda kuwa ombaomba. Baada ya kuona aibu tunapopewa pesa kama walivyo wenye akili, sisi tukipewa tunachekelea. NDIVYO TULIVYO.

    18. #55
      Baba Lao's Avatar
      Member Array
      Join Date : 12th May 2008
      Posts : 41
      Rep Power : 571
      Likes Received
      5
      Likes Given
      0

      Default Re: U.S. officials tour Dar Rapid Transport planned facilities

      Siyo U S wala nini.

      Ebu tuige kwa Wachina walivyo jizatiti kwenye huu usafiri wa BRT.Hakuna sababu ya kukimbilia Marekani.Huyo Cosmas Tekule aende China akajionee walivyojenga BRT na wanavyozimanage

    19. #56
      Baba Lao's Avatar
      Member Array
      Join Date : 12th May 2008
      Posts : 41
      Rep Power : 571
      Likes Received
      5
      Likes Given
      0

      Default Re: U.S. officials tour Dar Rapid Transport planned facilities

      Quote By Mkandara
      Lakini Marekani haijulikanai kwa kuwa na Public transit nzuri hata kidogo. Kuna states hazina usafiri mzuri na mipango ya Usafiri nxcchini humo ni tatizo sugu ambalo limewashinda viongozi kibao wa wajimbo..
      Kwa nini serikali yetu isitazame nchi zenye usafiuri mzuri kama vile UK, France, Canada na kadhalika badala ya Marekani
      ?.
      Mkuu gonga hapa ujionee wachina walivyo juu kwenye BRT.Nadhan utamshauri huyo Cosmas Tekule aende apate somo la jinsi gani unatakiwa kuzitunza hizo BRT.

      gonga hapa
      http://www.chinabrt.org/defaulten.aspx

    20. #57
      Kisusi Mohammed's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th August 2009
      Location : Kigamboni, Dar es salaam
      Posts : 328
      Rep Power : 563
      Likes Received
      24
      Likes Given
      39

      Default Mradi wa mabasi ya mwendo kasi

      Yawezekana habari hii sijaisikia kwa sababu inanipita au yawezekana haiongelewi. Kuna kipindi mwaka juzi na mwaka jana iliongelewa sana kwamba mradi huu ungeanza kutekelezwa kwa watu waliopo maeneo ya mradi kulipwa fidia ili kupisha utekelezaji wa mradi huo. Sasa imekuwa kipindi toka mradi huu uache kuzungumziwa. Nikiwa kama mkereketwa wa maendeleo nikaona si vibaya nikianika fikra zangu kwa wanaJF ili tujuzane na kujua exactly kinachoendelea kuhusu mradi huo.
      REALITY IS THE ONLY SOLUTION TO ALL THE PUZZLES!

    21. #58
      October's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th October 2009
      Posts : 2,045
      Rep Power : 903
      Likes Received
      44
      Likes Given
      49

      Default Re: Mradi wa mabasi ya mwendo kasi

      Yakhe Hujaona Mabasi makubwa yakielekea Katikati ya jiji?
      Huo ndio Mradi wenyewe kama huijui hii sirikali, we ungetaka mafisadi wapate wapi kisingizio cha kuchota hela kama sio kuja na mawazo mbofu mbofu kama haya? Ndo imetoka hivyo hakuna cha mabasi ya kasi wala nini, na mabilioni ya hela yameshatumika

    22. #59
      Kigogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th December 2007
      Location : Calabash
      Posts : 8,195
      Rep Power : 2095
      Likes Received
      1233
      Likes Given
      313

      Default Re: Mradi wa mabasi ya mwendo kasi

      Kisusi umenikumbusha...hakuna lolote katika huo mradi juzi nasikia wanataka kujenga barabara za juu kupunguza foleni..teh tehhhh kazi kweli kweli
      ______________________________ _
      Niko tayari kufa huku nimesimama kuliko kuishi huku nimepiga magoti....

    23. #60
      Magezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th October 2008
      Posts : 2,654
      Rep Power : 1073
      Likes Received
      33
      Likes Given
      50

      Default Re: Mradi wa mabasi ya mwendo kasi

      tangu lini mwizi akawaza kuwa na kilicho chake???

    Page 3 of 5 FirstFirst 12345 LastLast

    Similar Topics

    1. Replies: 217
      Last Post: 11th May 2013, 08:38
    2. Hii ya magari yaendayo kwa kasi imekaa je?
      By Shine in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 1
      Last Post: 21st September 2011, 15:47
    3. Replies: 70
      Last Post: 12th May 2011, 11:47
    4. Mabasi yaendayo kasi....!
      By jcb in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 7
      Last Post: 2nd March 2011, 12:15
    5. Kwa mtaji huu mradi wa Mradi wa mabasi yaendayo kasi jijini ni hadithi!
      By Tusker Bariiiidi in forum Business & Economic Forum
      Replies: 1
      Last Post: 3rd May 2010, 17:16

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...