Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Biashara ya Uchawi Tanzania

    Report Post
    Page 5 of 38 FirstFirst ... 3456715 ... LastLast
    Results 81 to 100 of 756
    1. #1
      Majimoto's Avatar
      Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 16
      Rep Power : 594
      Likes Received
      11
      Likes Given
      3

      Default Biashara ya Uchawi Tanzania

      Mikoa saba nchini Tanzania ndiyo tishio kwa kuwa na nguvu kubwa za uchawi
      1. Tanga ndio kinara
      2. Lindi unafuatilia
      3. Dar es Salaam
      4. Mtwara
      5. Tabora
      6. Kigoma
      7. Mwanza

      Mikoa yenye wachawi wengi, kwa maana kwamba karibu kila kaya kuna mchawi
      1. Sumbawanga (Rukwa) ndio kinara
      2. Ruvuma inafuatialia
      3. Mbeya
      4. Singida

      Mikoa ambayo wananchi wake ndio wateja wakuu wa wachawi
      1. Kilimanjaro inaongoza
      2. Morogoro inafuatilia
      3. Kagera

      Wateja wengine wa wachawi
      1. Wafanyabiashara
      2. Wasanii
      3. Kina mama wa nyumbani
      4. Wanafunzi wa shule za sekondari hasa wa kidato cha pili.
      Invisible, Gaijin, araway and 20 others like this.

    2. #81
      newmzalendo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Location : tanganyika
      Posts : 1,064
      Rep Power : 734
      Likes Received
      174
      Likes Given
      73

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      Duh! kwa hiyo ile story ya Manyoya pale salender ni ukweli.inamaana ni karibu na kituo cha police salenda bridge
      Quote By Majimoto View Post
      Lango la Mustallah liko baharini kati ya daraja la Salenda na bomba kubwa la maji machafu lililoingia ndani ya bahari.

    3. #82
      Twilumba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th December 2010
      Location : Kiseliani
      Posts : 2,194
      Rep Power : 886
      Likes Received
      481
      Likes Given
      76

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      Quote By Majimoto View Post
      LANGO KUU LA KUZIMU LA DAR ES SALAAM

      Kuzimu ni shimo la giza lililopo duniani katika ulimwengu usiooneka, hapo ndipo yalipo makao makuu ya shetani katika dunia tunayoishi. Shetani ameshikilia tawala za mataifa mengi, anamiliki utajiri na fahari zake zote na humpa ampendaye kwa sharti ni lazima umsujudie.

      Lango kuu la kuingilia kuzimu la Upanga Dar es Salaam linajulikana kwa jina la MUSTALLAH. Ndani ya shimo la Mustallah kuna aina kumi na mbili za majini makatili sana yanayoangamiza jamii ya watu wa jiji la Dar es Salaam. Wachawi wa nchi huenda mara kwa mara shimoni kuongeza nguvu za uchawi wao, kabla ya kuingia shimoni ni lazima ufunge kwa siku tatu. Hapa tunajifunza kuwa shetani naye huwa anafunga.

      Tuangalie sasa aina za haya majini ya Mustallah na kazi zao.

      1. Ratafari ni jini linalosimamia laana zote za ukoo.
      Wapo watu wanasema ukoo wetu unasumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu, kisukari, presha, kutokuolewa na mambo mengi ambayo utakuta ukoo unakuwa na tatizo moja linalofanana kwa kila mwanaukoo, hili jini ndilo linasimamia laana hizo zimalize ukoo hadi kifo.

      2. Muzaphari ni jini linalozuia mafanikio.
      Ukitupiwa hili jini, hutaweza kufanya jambo lolote ukafanikiwa. Ukikopa shs 500,000 bank kwa ajili ya kuanza bishara, utafilisika na kuingia kwenye deni, na dhamana yako uliyoweka bank kuuzwa. Ukitaka kujiendeleza kimasomo yatatokea matatizo mengi yatakayosababisha kusimamisha masomo yako.

      3. Latifu hili jini linasimamia mambo matatu, ufukara, mateso, na pesa zako kupotea katika mazingara ya ajabu ajabu.

      4. Jujan ni jini linalosababisha watu kula udongo.

      5. Jahad ni jini la kutorosha mali
      Makarani wa bank ndio hasa wanaoadhirika na hili jini, utakuta karani anafanya kazi kwa uangalifu mkubwa, lakini kila siku ana shoti ya pesa. Pia kwenye maduka ya kawaida na hasa supermarket.

      6.Hazinan hili jini linalosimamia pombe, uvutaji wa sigara, madawa ya kulevya na mirungi.

      7. Jube ni jini linalosimamia utasa, vipimo vya hospitali vitaonyesha kuwa huna tatizo lakini mtoto kamwe hapatikani.

      8. Sifafiru hili ni jini linalosimamia ukahaba. Likimwingia mtu yeyote, kwa siku atatembea na watu zaidi ya watano bila hamu ya mapenzi kumalizika.

      9. Subian hili ni jini linalosimamia ajali. Chakula cha hili jini ni damu.
      Linasababisha wanawake wasipate siku zao, wengine wanapata maumivu makali sana wakiwa katika hedhi, utasikia tumbo linakata kuanzia kushoto kwenda kulia na hali hiyo huendelea kwa muda hadi unanza kusikia maumivu makali ya mgongo.

      10. Sumri jini hili linanyonga watoto wakiwa tumboni kabla ya kujifungua, pia linajihusisha na kuchukua watoto hospitali kichawi.

      11. Munsar hili ni jini linalosimamia ndoa ya jinsia moja.
      mwanamke kwa mwanamke au mwanamume kwa mwanamume.

      12. Waidadat hili jini linasababisha vijana wa kiume kuvaa hereni, kusuka nywele na rasta.

      Haya majini yamesumbua familia nyingi kwa kiwango cha kutisha, kuyaondoa ni rahisi sana na kwa muda mfupi.
      Mkuu simulizi zinatisha... unafanyeje kupona na haya majitu?
      Intellectuals solve problems, geniuses prevent them.
      Albert Einstein.

    4. #83
      Mwelewa's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 5th January 2011
      Posts : 181
      Rep Power : 464
      Likes Received
      9
      Likes Given
      28

      Default

      Quote By Majimoto View Post
      Usijali jicho langu litakupa ulinzi.
      We Majimoto ni kwamba haya mambo unaexperience nayo au na wewe ni wakusimuliwa na kusoma vijarida na kuamini? Kama alivyosema VoiceofReason kila umuulizae atakwambia kuwa na yeye anasikia hebu tupe nyuzi za uhakika kwa mfano labda ulishawahi kuwa mchawi then umeamua kutoboa siri za kichawi au bado umo kundini ila umeamua kuvujisha data!
      Mi binafsi sina uhakika na haya mambo sijui kuna magari ya kichawi sijui kuna watu wanatembea barabarani halafu hawaonekani, sijawahi kuona wala kushuhudia tukio lolote la kichawi so siamini kabisa hayo mabo,,, truth is never told but must be realized!

    5. #84
      Chamoto's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th December 2007
      Posts : 1,387
      Rep Power : 1237
      Likes Received
      483
      Likes Given
      355

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      Haya mambo yapo mimi wakati mdogo (late eighties or early nineties) pale viwanja vya mnazi mmoja nilishuhudia Emmanuel Eni (yule Mnigeria aliyekuwa mchawi ila baadae akaokoka) akihubiri (akielezea maisha yake) jinsi alivyoishi maisha haya. Alisimulia hivyo vyou alivyopelekwa kusoma (INDIA) na jinsi alivyokuwa anasababisha ajali.

      Pia alieleze jinsi alivyolishwa maji ya maiti (yaani maiti inafukuliwa halafu inamwagiwa maji ili mchizi uwe na harufu ya maiti) ili anywe. Nakumbuka hata tuliwahi kununua kitabu chake na nilikisoma japo kuwa ni miaka mingi imepita (kama 20+) bado nakumbuka vipande vipande vya huo mkasa. (Mwenyewe nime shangaa kukumbuka hata jina lake na kugoogle)

      Haya mambo yanatisha sana ila ukiwa na Yesu huwezi kuogopa kwasababu aliyashinda yote hayo.

      Kuna link hii nimeipata toka google ambayo ni kitabu alichoandika yeye mwenyewe Emmanuel Eni kuhusu maisha yake kinaitwa:

      Delivered From The power Of Darkness

    6. #85
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,907
      Rep Power : 1857
      Likes Received
      626
      Likes Given
      421

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      LANGO LA KUZIMU LA PANGANI, TANGA

      Pangani ni mmoja ya miji ya zamani sana, upo kiasi cha kilomita 35 kutoka Handeni, kama unauwezo wa kuchapa mguu sawasawa itakuchukuwa muda wa masaa matatu hadi manne kufika Pangani. Maendeleo ya mji huu yamedumaa, sawasawa na miji mingine mingi iliyokaliwa na Waarabu, licha ya kuwa na vivutio vingi vya utalii.

      Ushirikina ndiyo shughuli kubwa katika mji huu, na hapo lipo lango la kuingilia kuzimu linalojulikana kwa jina la RAJUNI, lango hili lipo ndani ya bahari ya Hindi. Na linahudumiwa na majini makali kumi na mawili yafuatayo. (inashangaza sana kuwa malango yote ya kuzimu yanahudumiwa na majini kumi na mawili)

      1. Shadirun hili ni jini linalosimamia magonjwa ya ngozi, na fungus zisizosikia dawa na zinazowasha sana hasa katika sehemu za siri.

      2. Fadhan ni jini wanalotumiwa sana na wachawi kutambua kinga ya mtu, kabla ya wachawi hawajaenda kumfanyia ulozi. Hutumwa sana kwa walokole na huweza kutambua walokole feki na walokole wasioingilika.

      3. Baraji ni jini linalosimamia uvivu hasa kwa wanawake. Jini hili likitumwa kwa mwanamke anakuwa mvivu kweli kweli kwa kazi za nyumbani hadi kitandani.

      4. Shamsu ni jini linalo vaa umbile la binadamu. Utakuta msichana ni mzuri sana kwa sura na tabia lakini haolewi. Akitokea mvulana kumchumbia hili jini humwingia msichana na kumvika sura bandia, mvulana anapomtizama msichana anachanganyikiwa kwani anaona siye yule aliyekuwa anamtaka, hivyo anapigwa chenga hadi uchumba unavunjika. Akijitokeza kijana mwingine hali huwa ni ile ile ya kuachwa. Wasichana wengine hufunikwa kwa sura bandia kiasi kwamba tangu azaliwe hajawahi kukutana na mvulana walao wa kumtakia neno nakupenda.

      5. Amri ni jini linalosimamia hasira. Utakuta mtu anakuwa na hasira hadi anatetemeka na mapovu yanamtoka mdomoni.

      6. Tahimu anashughulika na kutambua nyota za watu, kisha wachawi huzichukuwa na kufanyia biashara.

      7. Tajirin hili ni jini linalosimamia utajiri. Masharti ya kulimiliki ni lazima uwape mtoto wako wa kuzaa au mke wako apooze upande au ufanye mapenzi na mama yako mzazi. Kisha ni lazima usaini mkataba wenye masharti magumu sana kama usilale kitandani, usipande gari, usile aina ya vyakula nk.

      8. Al Taliki hili ni jini la kupoteza watu. Kama kuna watu wanamtaka mtu fulani, wachawi hutuma hili jini nalo huvaa mwili wa binadamu na kwenda eneo au sehemu anapoishi huyo mtu. Likimwona huwita kwa vidole na watu wengine wanakuwa hawamuoni isipokuwa mlengwa peke yake, kisha huanza kumfuata jini kwa nyuma,jini akikimbia na huyo mtu naye hukumbia hadi anamfikisha kwa wachawi.

      9. Naruju ni jini linalosimamia lugha, wapo wanao nena lugha kwa kupagawa na majini na wapo wanao nena lugha kwa nguvu ya Mungu ambayo inawapa taabu sana kuzimu kwa moto unaounguza.

      10. Janjatus ni jini linalotumwa kuwafanya watu walale usingizi mzito wakati wa adhana na wakati wa mahubiri kanisani.

      11. Riaru jini hili likimwingia mtu anataka afanye kila kazi peke yake.

      12. Zaituni ni jini linalosimamia watoto wa kike kutembea kwa maringo na mikogo.
      Last edited by MAMA POROJO; 25th February 2011 at 05:12.
      MAJIDAI likes this.

    7. #86
      M-bongotz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th January 2010
      Location : Kwa Mtogole
      Posts : 1,527
      Rep Power : 785
      Likes Received
      246
      Likes Given
      13

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      Quote By Majimoto View Post
      Mbayuwayu miaka ya 1970 alipomaliza shule ya msingi, alionekana ni kijana aliyekuwa na bidii sana katika masomo yake darasani. Wazazi wake Mbayuwayu waliona itafaa kijana wao pia akajua fani ya uganga, hivyo walimtafutia mtaalamu ambaye alianza kumfundisha elimu ya jadi ya ulozi.

      Masomo aliyofundishwa na kuyaelewa vema ni jinsi ya kutengeneza majini, kuruka kwa ungo, kuchukuwa watu msukule na elimu ya nyota. Baada ya kuhitimu wazee walikutana kwenye mikutano ya wachawi usiku, Mbayuwayu naye alialikwa, alipongezwa sana kwa bidii aliyoonyesha kwenye masomo yake, na aliahidiwa tarehe ambayo atakabidhiwa cheti chake cha kuhitimu elimu ya ulozi.

      Tarehe ilipofika waliruka kwa ungo hadi Kisiju, Mkuranga, walipofika eneo la shughuli walikuta wapo vijana wenzake wawili ambao nao walikuwa wapate vyeti. Muda ulipowadia wazee waliwaita na kuelekezwa waende kwenye chungu kilichokuwa kipo jikoni. Walipokaribia chungu, walikuta ndani kuna nyama iliyokuwa inachemshwa, walielekezwa kila mtu akate kipande cha nyama ya kila kiungo na waweke kwenye sahani, walipofungua chungu, wakangundua kuwa ile nyama haikuwa ya mnyama bali ni nyama ya binadamu.

      Mbayuwayu bila kusita alitii amri ya wazee na akakata nyama za kila kiungo pamoja na supu yake, na kuanza kula. Wale vijana wawili walipogundua ile ni nyama ya binadamu waligoma kabisa kula, walilazimishwa na wazee lakini hawakukubali. Desturi za wachawi, damu na nyama za watu ni chakula cha kawaida, na ukishaingia kwenye ulozi unatakiwa uwe mtiifu na usitoe siri zao kwa mtu yeyote ambaye siyo mchawi.

      Wale vijana kwa daraja la uchawi walilokuwa wamefikia na viapo walivyoapa, adhabu waliyostahiki ilikuwa ni kifo, ilishangaza kidogo wale wazee vigagula walifanya mambo yao haraka na wale vijana walianguka chini wakiwa maiti.

      Wazee walimchukuwa Mbayuwayu usiku huohuo kwa usafiri wa ungo hadi makaburi ya Kinondoni, makaburi haya yapo karibu na baa ya Lang'ata ambapo wanazikwa Wakristo na Waislamu. Walikuta kaburi la Mkristo ambalo ni la siku kama tatu tangu marehemu azikwe. Wazee walifanya mambo yao ya kichawi na kaburi likafunguka, wakalipandisha juu jeneza, kisha wazee wakamwambia Mbayuwayu alivyunje kwa kulikanyaga kwa mguu wa kushoto. Jeneza lilipasuka na harufu ya kutisha ilitoka ndani, wale wazee walichukuwa kikombe kidogo kinachotumika kunywea kahawa mitaani, Wazee walimwambia Mbayuwayu achote majimaji yenye usaha toka ndani ya jeneza na anywe vikombe vitatu. Mbayuwayu bila ajizi wala kusita alitii amri, na kuchota ule usaha vikombe vitatu vilivyojaa na kunywa.

      Mbayuwayu alibaki anashangaa, alifikiri cheti alichoahidiwa kupewa ni sawasawa na cheti alichopewa alipomaliza elimu ya shule ya msingi, kumbe cheti ni kulishwa vyakula ambavyo hatavisahau maishani mwake.

      Baada ya hiyo karamu ya makaburini, wazee walimwambia Mbayuwayu, ajitayarishe kwani kesho yake watampeleka kumtambulisha kuzimu kwa mkuu, kupitia lango la kuzimu la Upanga ........................

      Je kuzimu ni wapi?
      Je unaweza kuingia kuzimu na kutoka?
      Ni nini kilimpata Mbayuwayu hadi akaokoka?

      Tafuta kanda ya DVD itwayo "Ushuhuda wa Mwisilamu (mchawi) Aliyeokoka"

      Kumbe kuna biashara inaendelea hapa
      Huwezi kumshawishi nyani mzee kwamba asali ni tamu kuliko ndizi mbivu.

    8. #87
      M-bongotz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th January 2010
      Location : Kwa Mtogole
      Posts : 1,527
      Rep Power : 785
      Likes Received
      246
      Likes Given
      13

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      Quote By Majimoto View Post
      Malaika Watakatifu, shetani, na majini ni baadhi ya viumbe wanaoishi kwenye ulimwengu usioonekana. Watu wengi wamekuwa wakifikiri kuwa ulimwengu usioonekana uko mbali sana na ulimwengu huu tunaoishi, ukweli ni kwamba wote tunaishi ulimwengu mmoja na barabarani huwa tunapishana, ingawa sisi hatuwaoni, lakini wao wanatuona kwa kila jambo tunalolifanya.

      Shetani anayo majeshi yake makubwa ajabu, kwa mfano hapo ulipo sasa kuna jeshi la shetani lenye askari wapatao 500 hadi 1000, wakigojea amri ya kushambulia, kuumiza na kuuwa.

      Wachawi wa nchi huwatumia sana hawa majini katika kutimiza dhamira zao mbaya za kudhuru maisha ya binadamu wenzao. Kimsingi hakuna tofauti kati ya wanaoitwa waganga wa kienyeji na wachawi (ni sawasawa na unaposema kuna askari na kuna polisi, wote ni walewale), watu wanapowaendea hawa wachawi kuaguliwa, huanza kwa kupiga manyanga na kuimba nyimbo za kichawi, wimbo huo ni wa kuita jini la utambuzi na tafasiri. Mtu anapowaza jambo fulani katika ulimwengu unaoonekana, katika ulimwengu usioonekana unaoongea kwa sauti kubwa kweli kweli, hili jini la utambuzi likifika linakaa karibu na wewe na kusikiliza kile unachowaza na kumweleza mchawi kwa lugha zao za kijini. Machawi akishaelezwa tatizo lako na jini, huanza kukueleza matatizo yako bila ya kukuuliza maswali yeyote, na watu wengi wamekuwa wakiishia kuwasifia sana hawa wachawi kuwa kabla hujasema anakuambia matatizo yako, asijue kuwa yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa akiongea kwa kuwaza.

      Kama umetupiwa jini, hawa wachawi hawana uwezo wa kuyaondoa majini yaliyowekwa mwilini mwako. Wanachofanya wanachukua jini mwingine mkubwa zaidi ya yule aliye ndani ya mwili wako, na anaelekezwa amtulize huyu jini asiendelee kufanya madhara ndani ya mwili wako. Jini mgeni naye inafika wakati anabadili tabia na kuanza kushambulia mwili wako, unapowaendea hawa wachawi wa nchi unavishwa jini mwenye nguvu zaidi kuwatuliza majini walio ndani ya mwili wako.

      Kadri unavyowaendea wachawi ndivo unaondoka na mtaji wa majini mengi mwilini mwako.
      Kwenye red hapo, hao lazima watakuwa ni FFU wa Bongo tu.
      Huwezi kumshawishi nyani mzee kwamba asali ni tamu kuliko ndizi mbivu.

    9. #88
      mageuzi1992's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th April 2010
      Posts : 2,057
      Rep Power : 878
      Likes Received
      145
      Likes Given
      115

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      Hii biashara ya uchawi inachangia sana tanzania kutoondelea

    10. #89
      carmel's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th August 2009
      Posts : 2,804
      Rep Power : 1075
      Likes Received
      202
      Likes Given
      128

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      Quote By Chamoto View Post
      Haya mambo yapo mimi wakati mdogo (late eighties or early nineties) pale viwanja vya mnazi mmoja nilishuhudia Emmanuel Eni (yule Mnigeria aliyekuwa mchawi ila baadae akaokoka) akihubiri (akielezea maisha yake) jinsi alivyoishi maisha haya. Alisimulia hivyo vyou alivyopelekwa kusoma (INDIA) na jinsi alivyokuwa anasababisha ajali.

      Pia alieleze jinsi alivyolishwa maji ya maiti (yaani maiti inafukuliwa halafu inamwagiwa maji ili mchizi uwe na harufu ya maiti) ili anywe. Nakumbuka hata tuliwahi kununua kitabu chake na nilikisoma japo kuwa ni miaka mingi imepita (kama 20+) bado nakumbuka vipande vipande vya huo mkasa. (Mwenyewe nime shangaa kukumbuka hata jina lake na kugoogle)

      Haya mambo yanatisha sana ila ukiwa na Yesu huwezi kuogopa kwasababu aliyashinda yote hayo.

      Kuna link hii nimeipata toka google ambayo ni kitabu alichoandika yeye mwenyewe Emmanuel Eni kuhusu maisha yake kinaitwa:

      Delivered From The power Of Darkness
      Nimesoma hiyo link aisee nimeogopa kumbe kuna mambo yanafanyika mengi sisi hatuna habari, Mungu na Atusaidie
      A gossip betrays a confidence; so avoid a man who talks too much.
      Proverbs 20:19

    11. #90
      Yo Yo's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 31st May 2008
      Posts : 10,895
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1356
      Likes Given
      2594

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      nasikia kikwete ana mchawi wake bagamoyo....pale jk unavyomuona ana hilizi kama 5 anatembea nazo....

    12. #91
      De Javu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2010
      Location : Onboard Pirate-ship off Somalia
      Posts : 267
      Rep Power : 521
      Likes Received
      22
      Likes Given
      6

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      Mkuu MMoto, wewe ni msaidizi wa sheikh YY nini? naona umebobea kwenye hili
      If you think EDUCATION is expensive....Try IGNORANCE and see how much it costs.

    13. #92
      Mlachake's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th October 2009
      Location : Loitokitok Kenya
      Posts : 1,855
      Rep Power : 872
      Likes Received
      518
      Likes Given
      348

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      Quote By Majimoto View Post
      Malaika Watakatifu, shetani, na majini ni baadhi ya viumbe wanaoishi kwenye ulimwengu usioonekana. Watu wengi wamekuwa wakifikiri kuwa ulimwengu usioonekana uko mbali sana na ulimwengu huu tunaoishi, ukweli ni kwamba wote tunaishi ulimwengu mmoja na barabarani huwa tunapishana, ingawa sisi hatuwaoni, lakini wao wanatuona kwa kila jambo tunalolifanya.

      Shetani anayo majeshi yake makubwa ajabu, kwa mfano hapo ulipo sasa kuna jeshi la shetani lenye askari wapatao 500 hadi 1000, wakigojea amri ya kushambulia, kuumiza na kuuwa.

      Wachawi wa nchi huwatumia sana hawa majini katika kutimiza dhamira zao mbaya za kudhuru maisha ya binadamu wenzao. Kimsingi hakuna tofauti kati ya wanaoitwa waganga wa kienyeji na wachawi (ni sawasawa na unaposema kuna askari na kuna polisi, wote ni walewale), watu wanapowaendea hawa wachawi kuaguliwa, huanza kwa kupiga manyanga na kuimba nyimbo za kichawi, wimbo huo ni wa kuita jini la utambuzi na tafasiri. Mtu anapowaza jambo fulani katika ulimwengu unaoonekana, katika ulimwengu usioonekana unaoongea kwa sauti kubwa kweli kweli, hili jini la utambuzi likifika linakaa karibu na wewe na kusikiliza kile unachowaza na kumweleza mchawi kwa lugha zao za kijini. Machawi akishaelezwa tatizo lako na jini, huanza kukueleza matatizo yako bila ya kukuuliza maswali yeyote, na watu wengi wamekuwa wakiishia kuwasifia sana hawa wachawi kuwa kabla hujasema anakuambia matatizo yako, asijue kuwa yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa akiongea kwa kuwaza.

      Kama umetupiwa jini, hawa wachawi hawana uwezo wa kuyaondoa majini yaliyowekwa mwilini mwako. Wanachofanya wanachukua jini mwingine mkubwa zaidi ya yule aliye ndani ya mwili wako, na anaelekezwa amtulize huyu jini asiendelee kufanya madhara ndani ya mwili wako. Jini mgeni naye inafika wakati anabadili tabia na kuanza kushambulia mwili wako, unapowaendea hawa wachawi wa nchi unavishwa jini mwenye nguvu zaidi kuwatuliza majini walio ndani ya mwili wako.

      Kadri unavyowaendea wachawi ndivo unaondoka na mtaji wa majini mengi mwilini mwako.
      Hapo kwenye nyekundi mapigo ya moyo yameruka, ukizingatia niko ofisini alone
      Knowledge is knowing that a tomato is a fruit; wisdom is knowing not to put it in a fruit salad.

    14. #93
      Mlachake's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th October 2009
      Location : Loitokitok Kenya
      Posts : 1,855
      Rep Power : 872
      Likes Received
      518
      Likes Given
      348

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      Jamani members! nilipoanza kusoma hii thread, Hili jicho kwenye avater ya majimoto lilikua linablink. sasa hivi liko kimya. au ndio majini yenyewe?
      MAJIDAI likes this.
      Knowledge is knowing that a tomato is a fruit; wisdom is knowing not to put it in a fruit salad.

    15. #94
      carefree's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 19th December 2010
      Posts : 219
      Rep Power : 474
      Likes Received
      9
      Likes Given
      3

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      kaazi kwelikweli kama utaenda kijiji kimoja ukajumuisha mkoa basi gt imepata maana mpya , no reserch no data jamaa kamwaga matokeo cjui ya nini

    16. #95
      ambili's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 233
      Rep Power : 487
      Likes Received
      13
      Likes Given
      31

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      Quote By Majimoto View Post
      Viongozi ni wateja wazuri, lakini idadi yao siyo kubwa
      wewe ni sangoma nini?
      "The laws of gravity cannot be held responsible for people falling in love"

    17. #96
      Katavi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 31st August 2009
      Location : Lyamba Lya Mfipa
      Posts : 19,931
      Rep Power : 16839
      Likes Received
      2648
      Likes Given
      2033

      Default

      Quote By Majimoto View Post
      LANGO KUU LA KUZIMU LA DAR ES SALAAM

      Kuzimu ni shimo la giza lililopo duniani katika ulimwengu usiooneka, hapo ndipo yalipo makao makuu ya shetani katika dunia tunayoishi. Shetani ameshikilia tawala za mataifa mengi, anamiliki utajiri na fahari zake zote na humpa ampendaye kwa sharti ni lazima umsujudie.

      Lango kuu la kuingilia kuzimu la Upanga Dar es Salaam linajulikana kwa jina la MUSTALLAH. Ndani ya shimo la Mustallah kuna aina kumi na mbili za majini makatili sana yanayoangamiza jamii ya watu wa jiji la Dar es Salaam. Wachawi wa nchi huenda mara kwa mara shimoni kuongeza nguvu za uchawi wao, kabla ya kuingia shimoni ni lazima ufunge kwa siku tatu. Hapa tunajifunza kuwa shetani naye huwa anafunga.

      Tuangalie sasa aina za haya majini ya Mustallah na kazi zao.

      1. Ratafari ni jini linalosimamia laana zote za ukoo.
      Wapo watu wanasema ukoo wetu unasumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu, kisukari, presha, kutokuolewa na mambo mengi ambayo utakuta ukoo unakuwa na tatizo moja linalofanana kwa kila mwanaukoo, hili jini ndilo linasimamia laana hizo zimalize ukoo hadi kifo.

      2. Muzaphari ni jini linalozuia mafanikio.
      Ukitupiwa hili jini, hutaweza kufanya jambo lolote ukafanikiwa. Ukikopa shs 500,000 bank kwa ajili ya kuanza bishara, utafilisika na kuingia kwenye deni, na dhamana yako uliyoweka bank kuuzwa. Ukitaka kujiendeleza kimasomo yatatokea matatizo mengi yatakayosababisha kusimamisha masomo yako.

      3. Latifu hili jini linasimamia mambo matatu, ufukara, mateso, na pesa zako kupotea katika mazingara ya ajabu ajabu.

      4. Jujan ni jini linalosababisha watu kula udongo.

      5. Jahad ni jini la kutorosha mali
      Makarani wa bank ndio hasa wanaoadhirika na hili jini, utakuta karani anafanya kazi kwa uangalifu mkubwa, lakini kila siku ana shoti ya pesa. Pia kwenye maduka ya kawaida na hasa supermarket.

      6.Hazinan hili jini linalosimamia pombe, uvutaji wa sigara, madawa ya kulevya na mirungi.

      7. Jube ni jini linalosimamia utasa, vipimo vya hospitali vitaonyesha kuwa huna tatizo lakini mtoto kamwe hapatikani.

      8. Sifafiru hili ni jini linalosimamia ukahaba. Likimwingia mtu yeyote, kwa siku atatembea na watu zaidi ya watano bila hamu ya mapenzi kumalizika.

      9. Subian hili ni jini linalosimamia ajali. Chakula cha hili jini ni damu.
      Linasababisha wanawake wasipate siku zao, wengine wanapata maumivu makali sana wakiwa katika hedhi, utasikia tumbo linakata kuanzia kushoto kwenda kulia na hali hiyo huendelea kwa muda hadi unanza kusikia maumivu makali ya mgongo.

      10. Sumri jini hili linanyonga watoto wakiwa tumboni kabla ya kujifungua, pia linajihusisha na kuchukua watoto hospitali kichawi.

      11. Munsar hili ni jini linalosimamia ndoa ya jinsia moja.
      mwanamke kwa mwanamke au mwanamume kwa mwanamume.

      12. Waidadat hili jini linasababisha vijana wa kiume kuvaa hereni, kusuka nywele na rasta.

      Haya majini yamesumbua familia nyingi kwa kiwango cha kutisha, kuyaondoa ni rahisi sana na kwa muda mfupi.
      We ni Shehe Yahya, au mwanae au msaidizi wake?

    18. #97
      Mgalanjuka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th August 2009
      Posts : 636
      Rep Power : 627
      Likes Received
      131
      Likes Given
      140

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      We mchawi Majibaridi.... Dowans wamelipwa? Wanafunzi wa shule wanaokaa chini tuwasaidieje waondokane na shida hiyo? Kina mama hospitalini wanaokosa dawa na matibabu?
      Chance favors the prepared mind.

    19. #98
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,907
      Rep Power : 1857
      Likes Received
      626
      Likes Given
      421

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      Baada ya biashara ya mitumba kuruhusiwa hapa nchini, wafanyabiashara wamekuwa wakiingiza kila aina ya nguo na vyombo vya aina mbalimbali.

      Moja wapo ya bidhaa ambayo inaingizwa kwa wingi nchini ni wanasesere (midoli) zikiwa katika maumbo mbalimbali kama mbwa, paka, watoto, nyoka, chura nk.

      Shetani akisaidiwa na wachawi wa nchi siku zote huwa wanatafuta milango ya kuingilia ndani ya maisha ya mtu, mara nyingi wachawi na majini huwa wanavaa maumbo ya panya, paka, mbu, nzi, mjusi kafiri kuingia kwenye makazi ya watu na kuwafanyia ulozi.

      Siku hizi baada ya watu wengi kununua na kumiliki madoli, utakuta chumba cha mapumziko kimepabwa kwa madoli aina mbali mbali, kama wana watoto, utakuta chumba cha kulala watoto kimejazwa madoli, watoto wakicheza nayo. Magari nayo yamekuwa yakipambwa kwa midoli ya kila aina.

      Wachawi wa nchi wakiingia ndani ya nyumba yako, wanachofanya ni kuweka majini yao ndani ya hiyo midoli au midoli sasa hivi ndiyo makazi ya wachawi na majini ndani ya nyumba yako, ndiyo maana tangu ununue hiyo midoli maradhi ya ajabu hayaishi nyumbani kwako.

      Huu ni ushauri wa BURE kwa yeyote mwenye kuwa na sikio la kusikia na asikie, mwenye macho ya kusoma na akasoma hii habari na kuielewa, ataamua mwenyewe linalokupasa kutenda.

    20. #99
      Kamongo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 20th March 2009
      Posts : 206
      Rep Power : 563
      Likes Received
      10
      Likes Given
      0

      Default

      [QUOTE=Majimoto;1669662]Baada ya biashara ya mitumba kuruhusiwa hapa nchini, wafanyabiashara wamekuwa wakiingiza kila aina ya nguo na vyombo vya aina mbalimbali.

      Moja wapo ya bidhaa ambayo inaingizwa kwa wingi nchini ni wanasesere (midoli) zikiwa katika maumbo mbalimbali kama mbwa, paka, watoto, nyoka, chura nk.

      Shetani akisaidiwa na wachawi wa nchi siku zote huwa wanatafuta milango ya kuingilia ndani ya maisha ya mtu, mara nyingi wachawi na majini huwa wanavaa maumbo ya panya, paka, mbu, nzi, mjusi kafiri kuingia kwenye makazi ya watu na kuwafanyia ulozi.

      Siku hizi baada ya watu wengi kununua na kumiliki madoli, utakuta chumba cha mapumziko kimepabwa kwa madoli aina mbali mbali, kama wana watoto, utakuta chumba cha kulala watoto kimejazwa madoli, watoto wakicheza nayo. Magari nayo yamekuwa yakipambwa kwa midoli ya kila aina.

      Wachawi wa nchi wakiingia ndani ya nyumba yako, wanachofanya ni kuweka majini yao ndani ya hiyo midoli au midoli sasa hivi ndiyo makazi ya wachawi na majini ndani ya nyumba yako, ndiyo maana tangu ununue hiyo midoli maradhi ya ajabu hayaishi nyumbani kwako.

      Huu ni ushauri wa BURE kwa yeyote mwenye kuwa na sikio la kusikia na asikie, mwenye macho ya kusoma na akasoma hii habari na kuielewa, ataamua mwenyewe linalokupasa kutenda.[/QUOTE kama huamini kuna uchawi njoo kibaha ufungue biashara ukutane na wagweno wachawi sana
      Advicer likes this.

    21. #100
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,907
      Rep Power : 1857
      Likes Received
      626
      Likes Given
      421

      Default Re: Biashara ya Uchawi Tanzania

      ZAZUNI Lango la kuzimu la Bagamoyo

      Mji wa Bagamoyo ni mji wa kizamani uliokaliwa na Waarabu, na maendeleo yake yalikuwa duni sana hadi siku za hivi karibuni, wageni walipoanza kuingia na kuwekeza katika mji huo.

      Lango la kuzimu la Zazuni liko ufukweni mwa bahari ya Hindi, likihudumiwa na majini kumi na mawili.

      1. Ruyat ni jini linalosimamia ndoto mbaya

      2. Al-Rahab ni jini linalosimamia shoti ya umeme na majanga ya moto, mfano wa majanga ya moto yaliyotokea katika mabweni ya kulala wanafunzi katika shule nyingi, jini hili lilihusika na kuwachukua watoto kuwapeleka msukuleni. Watoto hawa wote wapo hai, tangu vita hivi vya shetani vilipoanza mkoani Kilimanjaro katika shule ya wasichana ya Shauri Tanga, watoto hawa wanaishi katika mateso makubwa makubwa ajabu.

      3. Hadarash ni jini katili sana linaloua kwa kukata shingo na kunyonya damu ya mtu

      4. Anazihad ni jini linalokamata roho ya mtu, kisha mtu anaonekana amekufa, baada ya mazishi, wachawi huja na kusoma dua kaburi funguka na jini huiachia roho ya marehemu, ufahamu unapomrudia, wachawi huondoka naye.

      5. Zuzuk ni jini la maafa. Jini hili likiingia mtaani au kijijini, hutokea vifo vingi sana, kila siku watu wanazika.

      6. Munkar ni jini la makaburini. Jini hili linakutokea kwenye ndoto kama babu, bibi au mzazi wako waliokufa zamani, likiwataka mfanye jambo fulani au familia itaangamia. Kimsingi unapotekeleza maelekezo ya jini, mtakuwa mumejifunga wenyewe kwa kamba ya kifo toka kuzimu, na matatizo makubwa ya magonjwa na vifo huanza kwa familia.

      7. Tatazu ni jini la uasherati, unafanya tendo la ndoa bila kujali magonjwa au uko kwenye kipindi cha hedhi.

      8. Rabdi ni jini linalotumwa kwa Waislamu peke yake, kwa ajili ya kufanya fujo.

      9. Balshebe ni jini linalosimamia magonjwa na madhaifu ya mwili

      10. Sajidur ni jini linalosimamia pesa. Likitumwa kwako mshahara wako unapotea katika matumizi ya ajabu ajabu.

      11. Subrah ni jini linalosimamia mafarakano, na kutokuelewana kwa viongozi wa Makanisa.

      12. Lair Labi ni jini linalosimamia hofu na kukata tamaa.
      Last edited by MAMA POROJO; 28th February 2011 at 09:30.

    Page 5 of 38 FirstFirst ... 3456715 ... LastLast

    LinkBacks (?)

    1. 1st July 2012, 09:06
    2. 22nd May 2011, 19:01
    3. 6th May 2011, 13:26
    4. 11th March 2011, 20:24

    Similar Topics

    1. Biashara ya real estate tanzania
      By C.T.U in forum Business & Economic Forum
      Replies: 20
      Last Post: 2nd April 2013, 18:54
    2. Replies: 12
      Last Post: 17th September 2011, 17:27
    3. Biashara ya copper Tanzania
      By The Boss in forum Business & Economic Forum
      Replies: 1
      Last Post: 27th July 2011, 08:03
    4. Tanzania inashabikia uchawi
      By Obe in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 1
      Last Post: 28th June 2011, 13:27
    5. Uwekezaji na biashara inakuwa tanzania?
      By Haika in forum Business & Economic Forum
      Replies: 4
      Last Post: 28th January 2011, 13:13

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...