Mbayuwayu miaka ya 1970 alipomaliza shule ya msingi, alionekana ni kijana aliyekuwa na bidii sana katika masomo yake darasani. Wazazi wake Mbayuwayu waliona itafaa kijana wao pia akajua fani ya uganga, hivyo walimtafutia mtaalamu ambaye alianza kumfundisha elimu ya jadi ya ulozi.
Masomo aliyofundishwa na kuyaelewa vema ni jinsi ya kutengeneza majini, kuruka kwa ungo, kuchukuwa watu msukule na elimu ya nyota. Baada ya kuhitimu wazee walikutana kwenye mikutano ya wachawi usiku, Mbayuwayu naye alialikwa, alipongezwa sana kwa bidii aliyoonyesha kwenye masomo yake, na aliahidiwa tarehe ambayo atakabidhiwa cheti chake cha kuhitimu elimu ya ulozi.
Tarehe ilipofika waliruka kwa ungo hadi Kisiju, Mkuranga, walipofika eneo la shughuli walikuta wapo vijana wenzake wawili ambao nao walikuwa wapate vyeti. Muda ulipowadia wazee waliwaita na kuelekezwa waende kwenye chungu kilichokuwa kipo jikoni. Walipokaribia chungu, walikuta ndani kuna nyama iliyokuwa inachemshwa, walielekezwa kila mtu akate kipande cha nyama ya kila kiungo na waweke kwenye sahani, walipofungua chungu, wakangundua kuwa ile nyama haikuwa ya mnyama bali ni nyama ya binadamu.
Mbayuwayu bila kusita alitii amri ya wazee na akakata nyama za kila kiungo pamoja na supu yake, na kuanza kula. Wale vijana wawili walipogundua ile ni nyama ya binadamu waligoma kabisa kula, walilazimishwa na wazee lakini hawakukubali. Desturi za wachawi, damu na nyama za watu ni chakula cha kawaida, na ukishaingia kwenye ulozi unatakiwa uwe mtiifu na usitoe siri zao kwa mtu yeyote ambaye siyo mchawi.
Wale vijana kwa daraja la uchawi walilokuwa wamefikia na viapo walivyoapa, adhabu waliyostahiki ilikuwa ni kifo, ilishangaza kidogo wale wazee vigagula walifanya mambo yao haraka na wale vijana walianguka chini wakiwa maiti.
Wazee walimchukuwa Mbayuwayu usiku huohuo kwa usafiri wa ungo hadi makaburi ya Kinondoni, makaburi haya yapo karibu na baa ya Lang'ata ambapo wanazikwa Wakristo na Waislamu. Walikuta kaburi la Mkristo ambalo ni la siku kama tatu tangu marehemu azikwe. Wazee walifanya mambo yao ya kichawi na kaburi likafunguka, wakalipandisha juu jeneza, kisha wazee wakamwambia Mbayuwayu alivyunje kwa kulikanyaga kwa mguu wa kushoto. Jeneza lilipasuka na harufu ya kutisha ilitoka ndani, wale wazee walichukuwa kikombe kidogo kinachotumika kunywea kahawa mitaani, Wazee walimwambia Mbayuwayu achote majimaji yenye usaha toka ndani ya jeneza na anywe vikombe vitatu. Mbayuwayu bila ajizi wala kusita alitii amri, na kuchota ule usaha vikombe vitatu vilivyojaa na kunywa.
Mbayuwayu alibaki anashangaa, alifikiri cheti alichoahidiwa kupewa ni sawasawa na cheti alichopewa alipomaliza elimu ya shule ya msingi, kumbe cheti ni kulishwa vyakula ambavyo hatavisahau maishani mwake.
Baada ya hiyo karamu ya makaburini, wazee walimwambia Mbayuwayu, ajitayarishe kwani kesho yake watampeleka kumtambulisha kuzimu kwa mkuu, kupitia lango la kuzimu la Upanga ........................
Je kuzimu ni wapi?
Je unaweza kuingia kuzimu na kutoka?
Ni nini kilimpata Mbayuwayu hadi akaokoka?
Tafuta kanda ya DVD itwayo "Ushuhuda wa Mwisilamu (mchawi) Aliyeokoka"
Follow Us Here