LATEST ENTRIES
Gordon Kalulunga

Miaka 50 ya uhuru tunasumbuliwa na mbu wanaoishi siku 7!

March 14th, 2013 | by Gordon Kalulunga

TUMEFURAHIA na kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa taifa letu la Tanzania. Tumejiorodheshea mengi ya kujivunia. Yote yanaonekana. Wengi walifurahia lakini si wote tutanyamaza bila kuyasema mapungufu yanayoonekana.

Mariam Mkumbaru

Bunda: Ukosefu wa maji safi wapelekea wananchi kutumia maji machafu ya mitaro

March 14th, 2013 | by Mariam Mkumbaru

Wakazi wa wilaya ya Bunda  mkoa wa Mara, wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko katika kipindi hiki cha mvua, yanayosababisha na ukosefu wa maji safi na salama.

Gordon Kalulunga

Wakunga wa jadi 202 wapewa elimu ya afya Bunda

March 14th, 2013 | by Gordon Kalulunga

WAKATI mkoani Mbeya wakunga wa jadi wakizidi kudharauliwa na kukatazwa kuzalisha wajawazito, halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara imewapa mafunzo wakunga wa jadi 202 kwa ajili ya kuzalisha wajawazito wanaokwenda kujifungulia kwao.

Frank Leonard

Wajawazito watembea kilomita 16 kufuata huduma

March 13th, 2013 | by Frank Leonard

WAJAWAZITO wa kijiji cha Mgowelo kilichopo kata ya Mahenge wilayani Kilolo mkoani Iringa, wanalazimika kutembea kwa miguu zaidi ya kilomita 16 hadi kijiji cha Mtandika kufuata huduma za matibabu.

Gordon Kalulunga

‘’Hakuna anayejali vifo vya wajawazito na watoto wachanga!’’

March 12th, 2013 | by Gordon Kalulunga

HAKUNA anayejali kama mjamzito iwe kijijini au mjini anapotaabika na mimba yake wakati mtoto anayezaliwa ni mali ya taifa. Hakuna mtaalam wa afya anayejali kuona mjamzito anateseka na kushindwa kusukuma mtoto wakati wa kujifungua na hakuna anayejali kuona watoto wachanga hasa vijijini wanapokufa baada...

Belinda Habibu

Ukame, Ukosefu wa Chakula, vinavyoleta changamoto ya afya kwa waathirika wa UKIMWI huko Mwadui – Lohumbo

March 12th, 2013 | by Belinda Habibu

Ukame wa muda mrefu uliyoikumba vijiji vya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ni mwiba kwa waathirika wa virusi vya UKIMWI.

Mariam Mkumbaru

Utapiamlo wakithiri Wilayani Bunda, Mara

March 12th, 2013 | by Mariam Mkumbaru

Zaidi ya watoto 294 wapo hatarini kupoteza maisha kwa kuumwa ugonjwa wa utapiamlo katika kata ya Kibara na Kisori kwenye Jimbo la Mwibara wilaya ya Bunda mkoa wa Mara.

Belinda Habibu

Kishapu: Haya ndiyo yanayowapata Wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi Maghalata

March 12th, 2013 | by Belinda Habibu

Mto Sanga unaokatisha katika kijiji cha Maghalata kwa karibu km 13, huleta usumbufu kwa wanafunzi wanaotakiwa kuvuka wakapate elimu kwa upande wa pili ambako kuna shule.

Mariam Mkumbaru

Bunda: Sababu zinazowakimbiza wajawazito ‘Leba’ hizi hapa

March 12th, 2013 | by Mariam Mkumbaru

Sababu kubwa inayopelekea wajawazito kujifungulia kwa mkunga wa jadi pamoja na nyumbani, ni lugha chafu za manesi, ukosefu wa vifaa tiba na madawa muhimu kwa mjamzito baada ya kujifungua.

Belinda Habibu

Wasiwasi wa Maambukizi ya UKIMWI Kata ya Chome – Wilayani Same

March 12th, 2013 | by Belinda Habibu

“Hakuna sehemu yenye UKIMWI katika dunia hii kama ilivyo hapa Chome.”

Ni maneno ya Anna Clement anayeona mienendo ya wakazi wa eneo hili isivyokuwa mizuri, na kwa hali hiyo, maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI yatakuwa juu.

Mariam Mkumbaru

Jinsi Malaria inavyowamaliza watoto Bunda

March 11th, 2013 | by Mariam Mkumbaru

"Ilikuwa saa tatu asubuhi Mwajuma Ramadhani alianza kupata joto kali mwilini, mama yake Mwajuma akaenda duka la dawa kununua panadol akampa panadol joto likapungua baada ya saa moja, mtoto akawa anacheza vizuri alijua amepona,"alisema Winifrida Chales Mama yake Mwajuma.