Re: Obama in Ghana
Hii sio kali tu bali pia ni KUBWA KULIKO!!! Lakini haina tofauti na kauli za viongozi wengine wa kiafrika hususan Tz ambao huwa wanawakusanya vibaka na omba omba na kuwasweka ndani wakati wa ujio wa viongozi wa mataifa mengine hasa ya magharibi. Sina uhakika kama ndio "kufunika kombe ili mwanaharamu apite" au ni vinginevyo..lakini ukweli ni kwamba waafrika wengi tunaishi maisha ya kuwaridhisha wa-magharibi japo for sure they know that we are suffering a lot.
Huyu kiongozi ni mfano wa asilimia 99 ya viongozi wa Africa. Kwetu Tz hatuna jipya la kumfanya Obama atupe priority kama Ghana hasa kwenye suala zima la demokrasia, hapa ni corruption kwa kwenda mbele..kwani viongozi wa serikali wanaweza kuhamia kwenye eneo moja lanchi kwa muda katika kusaka ulaji kupitia chama lakini kunapotokea majanga kama ya MBAGALA au mengineyo viongozi wanaenda kwa mafungu tena kwa kusuasua au wasiende kabisa na bila sababu..
TULIPATA SIFA YA KUWA NCHI YA KWANZA KTK AFRIKA RAIS WETU KWENDA NYUMBA NYEUPE LAKINI TUMEKOSA SIFA YA KUWA WATU WA KWANZA KUMPOKEA RAIS KUTOKA NYUMBA NYEUPE, NI KWA VILE HATUSTAHILI NA HATUNA JIPYA ZAID YA KUJIKOMBA KWAO..
__________________
OmUkUnIrWa EmPhAbAcAcHuLoR
|