|
Quote: |
|
 |
|
|
sasa hii inajibu vipi neno "venture"... naona bado niko kwenye kipeo cha kwanza! |
|
|
|
|
--venture capitalist: bepari mhanga
--he/she ventured into something: alidiriki kufanya kitu fulani
--suicide terrorist: gaidi wa kujitoa mhanga
--suicide attempt: jaribio la kujiua
Hapo ndipo maana mimi nasema 'mhanga' laweza kuwa na nafasi yake kutegemeana na sentensi. Si lazima liwe na maana kamili katika kiingereza, as long as linaleta ladha nzuri na kueleweka kwenye kiswahili. Ndipo hapo unapokuta sisi hatuna she au he, lakini wao wanazo.
SteveD.
__________________
Jamii ijuayo uwiano thabiti kati ya dharau, ubinafsi, chuki na ustaarab dhidi ya jamii nyingine na baina ya watu wake ni jamii yenye maendeleo. Isiyojua ni dumazi. SD1-09.
Fikra ni nyenzo endelezi au potofu. Changamoto tuliyonayo ni kuchanganua na kutenganisha kati ya fikra endelevu na fikra potofu, kwani mwisho wa fikra ni matendo pale fikra hazibakii kuwa fikra. SD6-07Rev.2-09.