Re: Ukistaajabu ya Mussa...
Mama Bakari Mahiza,nafikiri umekalia kuti la kuanguka,CD unazozisikia ni ule mlio wa kuti kuanza kumeguka na kuanguka.Waandishi wa habari ambao ni kioo cha jamii ndio wanatujulisha juu ya kuti bovu linalotaka kuanguka.Isije ikawa ajabu kuti hilo litakapomeguka kabisaa! maana CD yake tumeshaicheza.Kumeguka kimya kimya wataumia wengi zaidi maana wanao umia na huo wimbo wa EPA, Richmond n.k. wanajua nyimbo hizo walizitunga vipi.Endelea kucheza mama ,na kama wewe hazikuhusu basi kaa chini na wenyewe wenye CD hizo wataendelea kunengua, kama waandishi wetu na vyombo vya habari wanavyo koleza vibwagizo!!!!!
|