|
Quote: |
|
 |
|
|
Nimeiona hiyo slogan mkuu.Sasa nasubiri mchango wako.Na wewe ni risk taker au..? |
|
|
|
|
Mkuu mimi naamini hivyo tu na daima nasimama katika slogan hiyo.
Sina ufanisi mkubwa katika maisha, lakini kuna mambo naweza eleza ama tunaweza kushirikishana.
Sipendi kuandika mengi sana kwa mkupuo lakini ningependa twende kwa njia ya mjadala.
Nianze kwa kusema kuwa ufanisi wowote unatokana na dhamira.
Watu wengi wana dhamira lakini dhamira zao si thabiti. Wakidhamiria jambo basi katikati wanaingiza mambo. Ukichanganya mambo mawili wakati mmoja haijalishi wewe ni Genius kiasi gani bado utaharibu sehemu moja tena uombee sehemu hiyo isiwe ile ambayo ndiyo ingekuinua.
Ni ukweli mwingine usiopingika kuwa dhamira yoyote inahitaji kujitoa. Hapo ndipo inaposimama slogan yangu. Maisha bila kuchukua risk hayafai hata kuishi!
Ni kweli; ukiwa na elimu nzuri basi maisha ya kati unaweza kuyaishi. Yani yale maisha ya kupata walau milioni mbili (pesa ya kitanzania) kwa mwezi na kuwa na uhakika wa watoto kula na kusoma shule za kawaida (bila ufisadi) na kijigari chako cha kutokea utakuwa nayo.
Wasomi wengi hawako tayari ku-risk, na walio-risk! Huwa sijui sababu nyuma ya hili lakini ukweli ni kwamba wengi wao wanaridhika na hali walizofikia na labda wanaogopa sana kuchafua CV zao. Ni wachache wenye kuthubutu! Hawa ni wazuri kwa maneno na wanaweza hata kuwa daraja la wale wenye uwezo wa kuthubutu kufanikiwa. Hawa huweza hata kuwapa mbinu za biashara wale wenye kuthubutu na kujikuta wanabakia na nafasi ya 'Consultants' (washauri?).
Wale wenye elimu za kati huwa wanajaribu kila jambo. Lile ambalo wanaona linawezekana hulipangia mikakati ya namna ya kulifanikisha na endapo wanadhamiria kabisa kufanikisha basi hufanikisha.
Nifupishe kwa sasa, niache nafasi ya wengine au hata mwanzisha mada kuongea ili twende sawa. Kama ni vitabu vya kusoma juu ya haya naweza kuwaletea lakini kwanza mada ikolee...