Re: Naomba maana ya maneno haya...
mpaka sasa neno "komputer" ni msamiati sahihi wa kiswahili. ni neno ambalo limetoholewa/ kukopwa kutoka katika kiingereza kama maneno mengine kama vile shati-(shirt), trekta-(tractor). kutohoa au kukopa maneno kutoka lugha nyingine, ni jambo la kawaida na katika lugha zilizo nyingi duniani zimetumia njia hii kujiongezea msamiati wake.
|