Re: Kampeni ya magazeti mapya ya karamagi & co. Dhidi ya jk
Mkuu umepiga ndipo! Umelonga kiuelewa. Umenikuna. Hawa watu hawahitaji fedha za mauzo za magazeti yao hayo ya udaku ambayo story zake nyingi ni za ubabaishaji tu. Wao wanauza message na soko lao kubwa ni Dar es Salaam. Fedha ya mauzo ni kwa ajili ya mamluki wao akina Prince Bagenda, Manyerere, Balile, na Muhingo. Magazeti haya yana kazi maalumu. Kwa mfano, gazeti la Nyundo lilipewa kazi moja tu kufanya: kumbomoa huyu kijana Nape kwa kumzulia kila jambo: si mtoto wa Nnauye, mpenda madaraka, mpuuzi, umri mkubwa utadhani Nchimbi ni teenager n.k. Kazi imefanyika, sasa gazeti hilo limesimama kidogo kusubiri assignment nyingine. TAIFA kazi kubwa ni kuwabamiza mastaa wa Mbeya na Kilimanjaro: Kimaro, Mwandosya, Kilango, Mwakyembe n.k. ndiyo maana magazeti mengi ya TAIFA yanauzwa Dar es Salaam, Mbeya na Kilimanjaro. Mkuchika aliingizwa mkenge na Salva na RA kuifungia MwanaHalisi. Walimpa shinikizo kubwa na kumpelekea ujumbe wa siri kuwa kabla ya kuwa Waziri alikuwa mfadhili wa MwanaHalisi. Of course huo ni uongo mkubwa, blackmail tupu. Lakini imefanyakazi.
|