Re: Kampeni ya magazeti mapya ya karamagi & co. Dhidi ya jk
WanaJF Mkandara, Pasco,Nurujamii, Rev. Kishoka na WildCat nimewasoma, nimewaelewa. Naomba mniamini, nilichoandika ni kweli kweli tupu. Kama mnakumbuka, nilishawadokeza kuwa nafanya kazi mojawapo ya kampuni kubwa ya RA. Nikigundulika ni mimi nachangia hapa JF, nitakuwa marehemu kesho ahsubuhi. Hawa watu wana mtandao wa nguvu sana, wana pesa na wana sauti kubwa kwenye vyombo vya usalama. Ni mtandao uleule uliompa ushindi JK. Wachache ni waadilifu, wamebaki na JK. Wengi wamefuata fedha za EPA, Richmond, Import Support - kikao kimoja tu cha KALOKIRO unalipwa 1m/= au 2m/=, utaacha kuunga mkono? Mwenyekiti wa operesheni nzima, kama nilivyosema awali, ni mzee wa Sumbawanga. Salva Rweyemamu hana record ya uzalendo, ni mamluki tu aliyeajiliwa na Richmond kwa msaada wa RA. Leo yuko Ikulu, atabadilika? Premy haelewi kuwa marafiki wa jana wa JK, ndo maadui wake leo. She is naive, anafuata mkumbo tu bila kuwa na bigger picture, bila kujua kuwa anamwumiza bwana mkubwa! Wahariri wa RAI wanajua hilo maana ndo wanaopokea "vigongo" kutoka kwa akina Salva. Niishie hapo maana naandika huku naangaza macho nisijeonekana Internet Cafe ahsubuhi nikichonga taarifa za JF.
Last edited by Invisible; 17th November 2008 at 10:21 AM..
Reason: Rechecking Personal details
|