Re: Mgomo wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini waandaliwa
Migomo kwa vyuo si jambo la kawaida kama ambavyo watu wanasema.tuangalie huu mgomo hawa wasomi wanataka nini na wamekiomba kwa muda gani mpaka sasa na bado selikeli imekaa kimya.It is just a very simple logic kwa nini serikali inakaa kimya kwa mambo ambayo ni ya msingi wakati upuzi inalipuka kama kifuu cha nazi.Hivi kuna haja gani ya kuwepo kwa bodi ya mikopo hapa Tanzania kwa sasa? iondoke haina maana yoyote zaidi ya kuendeleza ubaguzi.Tunaweza kulalamika kwamba kuna kuvuja kwa mitihani lakini tuangalie source ni nini?
Zamani ulikuwa ukipata division III na ukipata udahili ulikuwa unashangilia na unaaga nyumbani kuwa unaenda kusoma na hata kisaikolojia unajiandaa kwenda kusoma. je hiyo hali kwa sas ikoje wana ndugu? Hiyo mishahara wanayolipa wanafanyakazi wa bodi ni shilingi ngapi na matumizi ya kawaida ya kiofisi ni shilingi ngapi kwa mwaka achilia mbali vikao vya kila siku na night?
Inatakiwa ifike wakati tujikomboe kifkira, hizo bilions za walipa kodi zinazokwapulia na manyan'ganyi zingetumika vizuri, tusingeweza kuwalipia ada hao wanafunzi kweli jamani?
Tanzania tuna migodi mingapi na pesa inayopatikana huko inatumikaje kama siyo kuishia kwenye semina elekezi.Mimi naona wafanye mgomo mpaka kieleweke na hiyo bodi ifutiliwe mbali kabisa ili mtu akifaulu asiwekewe mizengwe tena na kuwa na mawazo jinsi ya kupata mikopo.Ni bora hata waongeze pay as you earn ili watu wasome bure na kupata taifa liloelemika lenye mapenzi na nchi yao.
|