Re: Mgomo wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini waandaliwa
Migomo mingine ni ya kujiumiza wenyewe. Vyuo havitobadilisha ratiba zao ipasavyo kuweza kurusu huu "mgomo", na wanafunzi wao wenyewe ndio wataopata shida ya kujaribu kujifunza vile ambavyo walitakiwa wafundishwe awali kufuatana na ratiba ya awali. Matokeo yake? Wanafunzi kushindwa kumaliza kusoma modules vizuri na labda kushindwa kufanya mitihani inavyotakikana.
Hivi wanafunzi wanataka serikali ifanyeje hasa ili iweze kupata ada zao kama sio kuzuia majibu yao ya mtihani?
|