JamiiForums |The Home of Great Thinkers - View Single Post - Kiini cha suplementary dept. Ya sociology
View Single Post
  #4  
Old 21st August 2008, 03:21 PM
Sipo's Avatar
Sipo Sipo is offline
Sipo is self-assured
JF Senior Expert Member
Points: 359,135, Level: 100 Points: 359,135, Level: 100 Points: 359,135, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Fri Jul 2008
Location: SIPAJUI
Posts: 2,167
Thanks: 382
Thanked 430 Times in 293 Posts
Rep Power: 26
Sipo will become famous soon enoughSipo will become famous soon enoughSipo will become famous soon enoughSipo will become famous soon enoughSipo will become famous soon enoughSipo will become famous soon enoughSipo will become famous soon enoughSipo will become famous soon enough
Default Re: Kiini cha suplementary dept. Ya sociology

[QUOTE=nguogani;270762]HI JEFF, nimejiunga rasmi leo ingawa nimekuwa msomaji wa mada mbalimbali kwenye hii forum. kilichonikuna ni mada ya sipo kuhusu sup hapo UDSM. kusema kweli imenigusa sana na nimesoma michango ya watu, kuna ya kuipa credit na kuna ya kuipuuza, ndio uhuru wa kusema huu. nianze kusema nami ni muathirika wa tatizo hili na si kweli kuwa hatusomi kama baadhi ya washiriki walivyosema ingawa ni kweli kuna ambao dhahiri hawasomi lakini haina maana ya kufanya generalization. kuna mambo makuu ninayotaka kusema:
1. sup ni kawaida na sehemu ya shule lakini kinachotokea hapa ni sup za lazima na za kukomoana baina ya lecturer na mwanafunzi, kwasababu mwalimu huyu toka mwanzo wa semister anasema ya kuwa hakuna wa kupata B+ hapa na kweli matokeo yakitoka ndivyo ilivyo. je hii ni sahihi kwenye ufundishaji?
2. somo la huyu mwalimu sio gumu kiasi hicho na kwa wale wanaokumbuka zamani lililkuwa likifundishwa na hayati Prof. Chachage na historia inaonyesha wanafunzi walielewa na aliyefeli alikubali kuwa mzembe. sasa huyu mwalimu toka apokee ni kilio na kusaga meno
3. hoja ya kusoma vitabu kwa huyu mwalimu sio sahihi kwani tulikuwa tunafuata mbinu zake zote za usomaji alizotaka yeye lakini kwakuwa alishapanga kukamata alikuwa haoni hivyo vitabu kwenye scripts wakati wa kusahihisha.
4. huyu sipo na mimi au wengine sio tunalalamika ila tunataka watanzania wajue kuwa kuna walimu wachache wanaharibu mfumo wa elimu Tanzania kwa malengo yao binafsi na kuyafanya maisha ya watoto wa maskini kuwa magumu, hata wale wanaojitahidi kwa kila hali.
5. tabia ya kukemea kwa huyu mwalimu pia ni kuwa na uhusiano na baadhi ya wanafunzi ambapo hudiriki hata kuwapa matokeo kabla hayajawa released. hii tumefanya uchunguzi na tunaongea kwa ushahidi madhubuti na sio bla bla.
6. kuhusu ku-appeal, jamani nyie sijui mnaujua ukweli kuhusu kuappeal, procedure ni nzuri lakini uhalisia sio hivyo. mwalimu huyu huyu anakwambia katika social sciences hakuna appeal na ukijaribu tu ni lazima udondokee pua. je nani wa kudhubutu. ebu fanyeni uchunguzi kabla ya kushauri jamani
7. halafu kuhusu dept kurudisha heshima yake, hivi heshima inakuja kwa kufelisha? mbona dept ya PSPA inaheshima yake kubwa tu na haijapatikana kwa kufelisha. hata dept ya GEOGRAPHY hipo juu sana kwa heshima ingawa sio kwa kufelisha.
8. halafu jamani hata mkuu wa dept ya sociology DR. MVUNGI, ABUU A.K alikuwa na kozi ngumu sana kuliko hata ya huyu DR lakini watu walisoma na wametoka waliokamatwa wanakiri kweli walifanya mistake sehemu fulani fulani.
9. jamani hakuna wanafunzi wanaosoma siku hizi kama dept ya sociology, hii ni kutokana na nature ya walimu lakini bado walimu wanawakamata vibaya mno. jaribuni kuangalia ratiba ya supllimentary hipo pale utawala inatisha sana upande wa hii dept. na hii inasababishwa na walimu kujisifu wanapokamata wanfunzi wengi kuliko wengine
10. hivi mnaposema degree sio vyeti mnamaanisha nini? M.A tutasomaje na GPA za 2.6 na 3.0 wakati vyuo vingine wanapata 3.5 mpaka 3.9. jamani elimu bongo inarudi nyuma. na kazi siku hizi zinapatikana kwa GPA nzuri na sio una nini kichwani, na mwajiri ataamini vipi una mambo kichwani wakati una GPA ya 2.0? GPA za sociology zinatisha sana na tutabaki tung'aa sharubu mtaani tu na wenye pesa ndio watakaosoma M.A ulaya kwa mapesa yao.

aisee nguogani umenigusa sana na naamini wewe umeweka mambo kiundani zaidi, na ndivyo ilivyo. Ila uliponiliza ni kwenye GPA jamani hapa ni tatizo, GPA ni mbovu ajabu, FAITH mwaka huu kuna first class moja, can you imagine? yaani grade C ndio fashion. Kwa hali hii masters tutasoma wapi??? hata vyuo vya nje SCHOLARSHIP hupati kwa LOWER SECOND... Hilo la vitabu nalo ni issue jamani....DR anasema msome kitabu cha KARL MARX & FREDRICK ENGELS ''collected works'' mtatafuta library yote hampati...na hapo mjue mnatakiwa mfanye BOOK REVIEW...kitabu kinakuja kupatikana kwake pekee bado wiki moja mkusanye kazi....kwanini msizime moto kama hali yenyewe ndio hiyo?. Na hapa pa kuappeal ndio kabisa umemaliza... kuna DR mmoja aliwahi kuniambia FASS hakuna APPEAL...labda uko ENGINEER NA B-COM. Nilimuelewa vizuri, nanyi fikirieni mtaelewa anamaanisha.
Aisee sipo sina mengi ila habari ndio hiyo na ukweli ndio huo... DR MVUNGI A.A.K (mkuu wa dept) lifanyie kazi hili vinginevyo maisha ya wanafunzi yataishia kuaribiwa na watu wachache ambao watoto wao wanasoma CAPETOWN UNIVERSITY na kwingineko.. Pia FAITH bigup dada unaifahamu vizuri dept na unaonyesha kweli umesoma kwenye ile dept inayoboa kuliko EPA au RICHMOND
Reply With Quote