Waungwana,
Suala la exemptions lina tofauti kidogo na hilo suala la bank kuu. Kiwango kilichotajwa kinatisha ingawaje mimi mwenyewe nimewahi kufaidika na hizo
exemptions. Lengo lake ni kupunguza gharama za wawekezaji, kwa mfano mimi
nimefaidika kwa kununua vifaa vya ujenzi bila VAT.
Tatizo ni pale ambapo hizo exemptions zinatumiwa vibaya na wajanja. Watu wanasema wanajenga hiyo miradi wakati hakuna na vifaa vinapotea.
Ila nijuavyo mimi sasa TRA wako macho sana na kila mara wanakuja kukagua
kuona kama hivyo vifaa vinatumika ipasavyo.
Idea yenyewe ni nzuri ila kama inatumia vibaya basi inapoteza maana nzima.
Nimeona nijisalimishe kwani katika hizo huenda kuna pesa ambayo mimi nime save ha haaa!!!
Kama exemptions zinatumika vizuri mategemeo ni kwamba hiyo miradi ikianza basi italipa kodi hata zaidi. Ukweli huenda ni tofauti na sisi wananchi ndio tunalipa hizo kodi huku wajanja hata hizo kodi wanaendelea kukwepa.
|