JamiiForums |The Home of Great Thinkers - View Single Post - Muungano na kero zake: Tuuvunje?
View Single Post
  #9  
Old 5th July 2006, 03:05 AM
Mkandara Mkandara is offline
Mkandara Aviator
JF Premium Member
Points: 580,378, Level: 100 Points: 580,378, Level: 100 Points: 580,378, Level: 100
Activity: 2% Activity: 2% Activity: 2%
 
Join Date: Thu Mar 2006
Location: T dot
Posts: 7,288
Thanks: 460
Thanked 741 Times in 324 Posts
Rep Power: 80
Mkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the rough
Default

Sam,

Maneno ya Jasusi ndiyo yangefunga kazi, lakini ndo...YANGE!

Zanzibar hatukumzaa sisi ni nchi ambayo inatakiwa kutambulika ndani ya muungano. Swala la Siasa lazima liongozane na Uchumi ktk muungano wowote wa nchi mbili, hii ni ndoa na huwezi kuleta mpango wa kienyeji. Tumeisha kula Yamin na haivunjiki bila kuwekwa ubani. Na ubani wenyewe ndio hiyo referendum. Kama bwana tunaweza kuwa na matumizi zaidi lakini haiwezekani tuseme hawana sauti kabisa. Tumefunga ndoa wenyewe tena kanisani ama msikitini, kilichotakiwa kilikuwa kuvuta ndani tu huku wake wa ndoa (mikoa) wakiwa na madaraka yao ya kiuchumi toka enzi zile za madaraka mikoani. Kwa hiyo Kisiasa ingejulikana tofauti na nje ya madaraka ya kiuchumi.

Nadhani swala hapa ni njia gani bora ktk muungano huu inapofikia kugawana mali. Kama ulivyosema asilimia 40.... toka wapi?.. hatuna serikali tatu. Mshikaji CCM sasa wanachemsha bara! Kama wanataka JM aonekane bingwa wa utawala basi hii ndiyo kaburi lao na kusema kweli nimepata habari za ndani kwamba wanaodai hasa kuwepo na wagombea binafsi wanatoka ndani ya CCM, hao mnaowasikia nje ni watu waliopandikizwa tu. Sii kazi mkasikia uchaguzi Ujao JM, Salim na Sumaye wanapigania kiti nje ya CCM kama wagombea binafsi. Kazi ipo na cheche za moto wanazianzisha wao wenyewe CCM. Habari hii ya 60 kwa 40 haikubaliki katu na vumbi litatoka bara.....Hiyo mikataba wananchi wapo radhi kuifumbia macho kwa sababu hawana elimu ya kufahamu hiyo mikataba lakini Mpango wa bara na visiwani hili swala jingine kabisa!
__________________
Exploration of reality
Reply With Quote