Sam,
Inasikitisha sana kusoma huo mswada unaotegemewa kufanywa sheria katika siku za usoni , swali langu mimi ni moja tuu Watanzania ni nani aliyetuloga ? Kwa nini atufikirii kabla ya kufanya maamuzi ?
Kweli , kuna haja ya kuwa rocket scientist kujua ya kuwa huo mswada ni ujinga na ni kuwatukana wazalendo ? Yaani mapato ya madini yagawanywe katika uwiano wa 60% bara na 40 % zanzibar ....Ni vigezo gani wametumia kupata hizi figure ? kwanza zanzibar ina population ya watu wangapi .
Sam , naona utakuwa unaumiza kichwa tuu . Hawa viongozi awajali watu wa kawaida wanachodai ni masilahi yao binafsi ! siasa za bongo ni upotevu wa muda kwani wananchi wako so dormant na mara nyingi wanaishia kulalamika tuu .kikifika kipindi cha uchaguzi wanapitishiwa mswada wa kuwapa pilau " wanahongwa pilau " then wanawachagua kwa asilimia 80%.
|